Upinzani na serikali kuunda kamati Misri | Habari za Ulimwengu | DW | 07.02.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Upinzani na serikali kuunda kamati Misri

Wawakilishi wa wanasiasa wa upizani na Makamu wa rais mpya wa Misri wamekutana na kuafikiana kuunda kamati maalum itakayozidurusu upya sheria za nchi na katiba.

default

Viongozi wa upinzani na serikali kwenye kikao,Cairo

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Misri Magdi Radi,kamati hiyo itawaleta pamoja wanasheria wa ngazi za juu na wanasiasa watakaokuwa na wajibu wa kutoa mapendekezo ya mageuzi ya katiba na taratibu bungeni ifikapo mwanzoni mwa mwezi ujao wa Machi.

Kamati nyengine ya pembeni itakuwa na wajibu wa kuundoa mkwamo wa kisiasa uliopo kadhalika kuzipa msukumo harakati za kuwa na uhuru zaidi wa kupata maelezo kwenye mtandao.  

Ägypten Proteste Chaos Flash-Galerie

Waandamanaji wanaompinga Rais Hosni Mubarak wakiwa uwanja wa Tahrir,tarehe 6 Februari

Wapinzani wa serikali wamekuwa wakiandamana tangu wiki mbili zilizopita wakiwa na lengo la kumshinikiza Rais Hosni Mubarak ajiuzulu baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 30.Kwa upande wake Rais Mubarak aliye na umri wa miaka 82 anashikilia kuwa kamwe hatojiuzulu mpaka uchaguzi utakapofanyika ifikapo mwezi wa Septemba kama ilivyopangwa.

DW inapendekeza

 • Tarehe 07.02.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/10BsS
 • Tarehe 07.02.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/10BsS

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com