1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani katika jimbo la Catalonia kabla ya kura ya maoni

Zainab Aziz
2 Oktoba 2017

Vuguto lapamba moto katika miji ya Uhispania kabla ya kura ya maoni juu ya uhuru wa jimbo la Catalonia kufanyika hapo kesho Jumapili.

https://p.dw.com/p/2l1It
Spanien Madrid Demonstration für Einheit Spaniens
Picha: Reuters/R. Marchante

Watu wanaounga mkono kujitenga kwa jimbo la Catalonia nchini Uhispania tayari wameanza kuelekea katika maeneo ya kupigia kura kwa ajili ya kura ya maoni iliyopangwa kufanyika kesho Jumapili.  Serikali kuu ya Uhispania ambayo tayari imetuma maelfu ya askari polisi kwenye jimbo hilo inasisitiza kuwa kura hiyo haitafanyika. Hadi kufikia sasa polisi imevigunga vituo vya kupigia kura 1,300 kati ya vituo 2,315  Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono kura hiyo ya maoni wamekusanyika mjini Barcelona kwa ajili ya kampeni ya mwisho ya kuwashawishi watu kupiga kura ya ndiyo ili kuunga mkono hatua ya kujitenga kwa jimbo hilo.  Serikali ya jimbo la Catalonia imesema matayrisho kwa ajili ya kura hiyo ya maoni yamekamilika.

Waandamanaji wamiminika mijini

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika katikati ya jiji la Barcelona kwenye mkutano wa mwisho kabla ya kufanyika kura hiyo ya maoni ya hapo kesho tarehe Mosi mwezi Oktoba wafuasi hao walikuwa wanapeperusha bendera za Estelada, hiyo ni alama inayoashiria uhuru wa kujitenga na Uhispania. kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont, aliwambia wafuasi waliokuwa wamejawa na furaha kwamba "katika nyakati hizi zinazotawaliwa na hisia”, tulidhani tunachokifikiria  kilikuwa ni ndoto tu lakini kumbe ni kitu ambacho tunaweza kukifikia."

Polisi wa Uhispania

Polisi wa nchini Uhispania wamekiweka chini ya ulinzi kitengo cha mawasiliano cha serikali ya jimbo la Catalonia.Wafuasi  wa kura ya ndiyo wanasema wako tayari kwa makabiliano na polisi ambao wameagizwa na serikali kuhakikisha kuwa kura hiyo ya maoni haifanyiki. Chanzo kimoja cha serikali kimefahamisha kwamba polisi watawaondoa wafuasi wanaotaka uhuru wa jimbo la Catalonia kutoka kwenye vituo vya kupigia kura hapo kesho siku ya Jumapili lakini chanzo hicho hakikutoa maelezo zaidi. Serikali ya Uhispania imesema wafanyakazi wa kujitolea katika kura hiyo ya maoni ya hapo kesho lazima wafahamu kuwa hilo ni kosa na kwamba wanaweza kutozwa faini ya hadi Dola za Kimarekani 354,360 sawa na Euro 300,000.

Mwandishi: Zainab Aziz/APE/AFPE

Mhariri: Isaac Gamba