1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upigaji kura waendelea DRC

28 Novemba 2011

Raia katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wanaendelea kumiminika vituoni kushiriki katika uchaguzi mkuu wa kuchagua rais, baada ya wagombea kufanya kampeni kali mjini Kinshasa iliokumbwa na vurugu.

https://p.dw.com/p/13IIZ
Wapigakura wakizungumza kwa hasira na msimamizi wa uchaguzi kwa kuchelewesha vifaa vya kura.
Wapigakura wakizungumza kwa hasira na msimamizi wa uchaguzi kwa kuchelewesha vifaa vya kura.Picha: AP

Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa saa 1:00 na vinatarajiwa kufungwa saa kumi na moja jioni. Rais Joseph Kabila, anayepigania muhula wa pili madarakani, ana kibarua kigumu kumenyana na wagombea wengine kumi akiwemo mpinzani wake mkuu mwanasiasa mkongwe nchini humo Etienne Tshisekedi

Mwandishi wetu wa Kinshasa, Saleh Mwanamilongo, na John Kanyunyu wa Goma, wanaeleza sura halisi ya mambo yanavyoendelea katika uchaguzi huo.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri Mohammed Abdulrahman.