1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upigaji kura waanza.

2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVez

Moscow.Uchaguzi wa bunge nchini Urusi umeanza huku kukiwa na ulinzi mkali katika eneo la mashariki ya nchi hiyo. Kura ya kwanza zimepigwa huko katika mji wa Chukotka katika mpaka na jimbo la Marekani la Alaska na pia katika rasi ya Kamchatka. Kituo cha mwisho cha kupigia kura kitafungwa katika eneo la Kalinigrad lililoko katika bahari ya baltic jioni ya Jumapili. Watu wenye siasa za wastani nchini Urusi wamemshutumu rais Vladimir Putin kwa kutumia vibaya madaraka yake na kusema maafisa waliwasumbua wapinzani wakati wa kuelekea katikla uchaguzi. Chama cha United Russia cha Putin kinatarajiwa kushinda kwa wingi mkubwa, na kumruhusu kuongeza ushawishi wake hata baada ya kuondoka madarakani kama rais mwaka ujao. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameshutumu uchaguzi huo, akilenga kuhusu idadi ndogo ya waangalizi wa uchaguzi huo.