1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umojawa Islamic jihad wachukua dhamana

12 Septemba 2007

Umoja huo umejitwika jukumu la njama ya kushambulia kambi ya wanahewa ya Marekani huko ramstein,Ujerumani-njama iliozimwa kabla kufanyika.

https://p.dw.com/p/CH8G
Waziri Schauble
Waziri SchaublePicha: AP

Wiki moja baada ya kutiwa nguvuni kwa washukiwa 3 wa ugaidi nchini Ujerumani,kikundi cha Uzbekistan chenye mafungamano na mtandao wa Al Qaeda,kimejitwika dhamana kuwa nyuma ya njama ya kuihujumu kambi ya wanahewa wa Marekani nchini Ujerumani huko Ramstein na vituo vyenginevyo humu nchini.Njama hiyo ilizimwa na vyombo vya usalama.

Wizara ya ndani ya ujerumani mjini Berlin imearifu kwamba kikundi hicho kilipanga halkadhalika kuzihujumu afisi-ndogo za ubalozi za Marekani na Uzbekistan ziliopo humu nchini.

Kikundi cha Islamic Jihad Union ,kimechukua dhamana hii kupitia taarifa yake kwenye mtandao.Hujuma hii kwa kweli,ilipangwa ifanyike mwishoni mjwa mwaka huu wa 2007.

Islamic Jihad ikaarifu zaidi madhumuni ya hujuma hizo ilikua kuishinikiza Ujerumani kuyaondoa majeshi yake yaliowekwa katika kambi ya Termez,kusini mwa Uzbekistan.Ujerumani inaitumia kambi hiyo ya termez kwa shughuli zake za kijeshi katika nchi jirani ya Afghanistan ambako ina askari 3000 wanaotumika katika kile kikosi kinachoongozwa na NATO.

Mwanzoni mwa mwaka 2004, kikundi hiki kilijitwika jukumu la masham,bulio yaliofanyika huko Basare na kwenye vituo vya polisi nchini Uzbekistan.Jumla ya watu 47 waliuwawa.

Miezi michache baadae,wapiganaji wake wa kujitoa mhanga walijiripua katika hujuma dhidi ya balozi za Marekani na Israel,kwenye mji mkuu Tashkent.

Awali, Umoja huu wa Islamic Jihad wa Uzbekistan, ukilenga mashambulio yake ndani ya Uzbekistan kama vile kutaka kumpindua rais Karimov wa Uzbekistan,anaeshirikiana na Marekani.

Sasa baada ya kutiwa nguvuni nchini Ujerumani kwa washukiwa ugaidi 3-wawili kati yao wakiwa raia wa kUjerumani na 3 mturuki,idara za usalama za Ujerumani, imengamua kwamba kikundi hiki kimetanua harakati zake hadi Ujerumani.

Mshtaki-mkuu wa serikali Bibi Monika Herms anahisi washukiwa hao 3 waliotiwa mbaroni ni wanachama wa tawi la Ujerumani la Umoja wa Islamic Jihad,Uzbekistan.

Hata waziri wa ndani wa ujerumani Bw.Wolfgang Schaüble hana shaka tena:

“Umoja wa Islamic Jihad,ndio uliongoza njama hii kutoka Pakistan na ndio ulioamrisha wakati sasa umewadia kuhujumu.Na ndio pia uliowapa vijana hao mafunzo.”

Katika ripoti ya siri,idara za usalama za Ujerumani ,zimearifu washukiwa hao 3 ,walipewa mafunzo na wafuasi wa Umoja wa Islamic Jihad,nchini Pakistan.Kwa muujibu wa taarifa hizo,kikundi hicho kina mafungamano pia na mtandao wa Al Qaeda.

Na ingawa si desturi kwa vikundi hivyo vya kigaidi kuchukua dhamana ya hata hujuma zisizofanikiwa, waziri wa ndani wa Ujerumani Bw.Schauble,anawaamini mabingwa wake wa usalama katika kituo kikuu cha mtandao mjini Berlin.Ni wao walioichambua taarifa ya kuchukua dhamana ya njama hiyo iliotolewa na Umoja wa Islamic Jihad .

“Mabingwa wanaamini hiyo ni taarifa sahihi ya Umoja huo.”

Umoja huo wa Islamic Jihad, umebainisha dhahiri-shahiri unachotaka-nacho ni kufungwa vituo vya kambi za waanhewa zinazotumiwa na Jeshi la Ujerumani-Bundeswehr,huko Thermes, Uzbekistan.Ni katika uwanja huo,madege ya aina ya Airbus yaweza kutua yakitokea Ujerumani.