1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waupongeza mpango wa Ugiriki

Kabogo Grace Patricia4 Machi 2010

Ni mpango wa kupunguza matumizi yake ya fedha ya euro bilioni 4.8

https://p.dw.com/p/MJAi
Waziri Mkuu wa Ugiriki, George Papandreou (Shoto) akizungumza na Kamishna wa Umoja wa Ulaya wa nasuala ya uchumi, Olli Rehn (Kulia).Picha: AP

Umoja wa Ulaya umepongeza mpango wa Ugiriki wa kupunguza matumizi ya fedha ya euro bilioni 4.8 ili kujaribu kupunguza nakisi kubwa ya bajeti yake na kupata hakikisho la kusaidiwa kifedha na mataifa ya Ulaya. Mpango huo unajumuisha kupunguza gharama za sekta ya umma, kusitisha malipo ya uzeeni na kuongeza kodi.

Kamishna mpya wa masuala ya nishati wa Umoja wa Ulaya, Guenther Oettinger ameonyesha uwezekano wa umoja huo kuisaidia Ugiriki, lakini amesema nchi hiyo lazima itekeleze jukumu lake kwanza. Ugiriki imesema italigeukia Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF kama Umoja wa Ulaya utashindwa kuisaidia.