Umoja wa Ulaya washutumu mashambulio nchini Iraq | NRS-Import | DW | 23.12.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Umoja wa Ulaya washutumu mashambulio nchini Iraq

Umoja wa Ulaya umeshutumu vikali mashambulio ya mabomu jana mjini Baghdad na kusababisha watu 67 kuuwawa.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Catherine Ashton

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Catherine Ashton

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ameshutumu vikali mashambulio ya jana Alhamis mjini Baghdad ambapo watu 67 wameuwawa na amewataka viongozi wa Iraq kuanzisha majadiliano mara moja ili kutatua tofauti zao. Katika taarifa Ashton ameshutumu upotevu wa maisha uliosababishwa na magaidi wanaotumia hali tete iliyopo ya kisiasa. Miripuko ilitokea katika maeneo 14 tofauti, ililenga maeneo ya Washia. Polisi ya Iraq inatuhumu wanamgambo wa Kisunni kuwa wanahusika na mashambulio hayo. Waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki ameahidi kuwa washambuliaji hatawaruhusiwa kuleta athari yoyote katika hatua za kisiasa, wakati spika wa bunge Osama al-Nujaifi ameshutumu mashambulio hayo, ambayo amesema yanatishia umoja wa kitaifa.

 • Tarehe 23.12.2011
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Maneno muhimu Iraq
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13Y3y
 • Tarehe 23.12.2011
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Maneno muhimu Iraq
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13Y3y

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com