1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wakubaliaana juu ya uhamiaji

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYkO

BRUSSELS

Mawaziri wa sheria na mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels Ubelgiji wamekubaliana juu ya haja ya Umoja wa Ulaya kuwavutia wafanyakazi mwenye ujuzi.

Hata hivyo Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ni miongoni mwa wale wenye mashaka makubwa juu ya pendekezo la Kadi ya Buluu ambayo ni viza ya uhamiaji kwa wasiokuwa raia wa Umoja wa Ulaya.

Uhispania na Ugiriki zimesisitiza umuhimu wa kuzuwiya kumiminika kwa wahamiaji wasio halali wanaovuka bahari ya Miditerranean na kuingia Ulaya wakati Uingereza imependekeza kukubali wahamiaji kwa kukidhi tu mahitaji maalum ya nchi binafsi wanachama wa Umoja wa Ulaya.