Umoja wa mataifa:Jeshi nchini Philippines lahusishwa na mauaji | Habari za Ulimwengu | DW | 21.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umoja wa mataifa:Jeshi nchini Philippines lahusishwa na mauaji

Mchunguzi maalum wa Umoja wa mataifa amelishutumu jeshi la Israel kwa “ udanganyifu”, kuhusika na mlolongo wa mauaji ya kisiasa tangu 2001. hayo yanafuatia kwa orodha iliotolewa na shirika la haki za binaadamu nchini humo ya watu 832 wanaodaiwa wameuwawa, ikiwa na pamoja na vifo vya wanaharakati 356 wa siasa za mrengo wa shoto. Mchunguzi huyo wa umoja wa mataifa Philip Alstrom alikataa kutaja orodha kamili ya waliouwawa, lakini amesema jeshi lilihusika na sehemu kubwa ya mauaji hayo.

Alisema amri haikutoka kwa Rais Gloria Aroyo, lakini serikali yake imeruhusu kuwepo kwa hali ya ukandamizaji na ambayo baadhi ya wakati imesababisha mauaji. Polisi nchini Philippines, imeshindwa kufuatilia vifo vinane kati ya kumi vilivyotokea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com