1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa walaani machafuko ya Kenya

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3gc

NEW YORK:

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani machafuko yanayoendelea nchini Kenya.Baraza hilo limetoa mwito kwa pande hasimu nchini Kenya kutenzua mgogoro huo kwa njia ya majadiliano.Wakati huo huo,Baraza hilo limemuunga mkono aliekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anaeongoza majadiliano kati ya serikali na upande wa upinzani.

Wakati huo huo,ujumbe wa Umoja wa Mataifa umewasili nchini Kenya kuchunguza madai ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika machafuko yaliyoripuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais Desemba 27.Kwa mujibu wa Msalaba Mwekundu,zaidi ya Wakenya 1,000 wameuawa na kama 300,000 wengine wamepoteza makazi yao katika machafuko hayo.