1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waiondolea vikwazo Libya

Sudi Mnette17 Desemba 2011

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamuru mali ya benki mbili zilizokuwa zikidhibitiwa na Muammar Gaddafi na baadaye kuzuiliwa na Umoja huo, sasa zinapaswa kuachiwa huru.

https://p.dw.com/p/13Uis
Kiongozi wa Baraza la Mpito la Libya, Mustafa Abdul Jalil.
Kiongozi wa Baraza la Mpito la Libya, Mustafa Abdul Jalil.Picha: picture-alliance/dpa

Hatua hiyo imetajwa kuwa na lengo la kusafisha njia katika kuisadia serikali mpya itakayopata zaidi ya dola bilioni 40, ili ziweze kufanikisha ujenzi upya wa taifa hilo. Baraza la Usalama lilizuia mali za taasisi tano muhimu za Libya mapema Machi mwaka huu. Baada ya kifo cha Gaddafi na kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenywe vilivyodumu kwa miezi minane, Baraza hilo lililegeza kamba kwa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi. Hata hivyo, mali za Benki Kuu na Benki ya Nje zilikuwa bado zimezuiwa kabla ya mwezi Machi, ziliendelea kuzuiliwa hadi jana.