1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika wakabidhi madaraka ya ulinzi wa amani kwa UM.

1 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CieD

Darfur.

Katika jimbo la Sudan la Darfur , umoja wa Afrika umehamisha mamlaka yake kwa jeshi la pamoja na umoja wa Afrika na umoja wa mataifa la kulinda amani. Hatua rasmi ya makabidhiano imekuja katika sherehe iliyofanyika katika makao makuu ya ujumbe huo mpya nje ya mji wa El Fasher. Hatua hiyo inafuatia miezi kadha ya mbinyo wa kimataifa dhidi ya rais wa Sudan Omar al-Bashir kuruhusu majeshi ya umoja wa mataifa kuingia nchini humo. Ujumbe huo katika jimbo la Darfur , ambao utajulikana kama UNAMID utakuwa mkubwa kabisa kwa umoja wa mataifa ukiwa na wanajeshi 20,000 , polisi 6,000 na wafanyakazi wa kawaida. Hadi sasa ni kiasi cha wanajeshi 9,000 ambao wako katika jimbo hilo.