1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umma usiogope serikali - Serikali iogope umma

24 Oktoba 2011

Uchaguzi wa Tunisia, mzozo wa madeni katika kanda inayotumia sarafu ya Euro ni baadhi tu ya mada zilizogonga vichwa vya habari katika magazeti ya Ujerumani leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/RscD
Tunis Testwahl in einem Wahllokal, 16.10.2011; Copyright: DW/Mounir Souissi
Watunisia wamepiga kura kuchagua baraza la kutunga katiba ya taifaPicha: DW

Tunaanza na uchaguzi uliofanywa hapo jana nchini Tunisia ambako ndiko kulikoanzia vuguvugu la mageuzi la nchi za Kiarabu. Gazeti la OFFENBURGER TAGEBLATT limeandika hivi:

"Wimbi la demokrasia linaendelea kuenea kila pembe ya dunia. Tunisia kumefanywa uchaguzi huru kwa mara ya kwanza. Umma wa Afrika Kaskazini umewatimua madikteta wao kama ilivyotokea hivi karibuni nchini Libya. Demokrasia ni mfumo unaowavutia watu masikini na waliokuwa wakikandamizwa. Hiyo haishangazi, kwani kwenye mtandao na televisheni, wanaona maisha ya neema katika nchi za magharibi. Kwa umma huo, demokrasia humaanisha maisha ya neema. Lakini maisha ya neema hayapatikana hivi hivi."

Gazeti la KÖLNER STADT-ANZEIGER likiendelea na mada hiyo, limenukuu kauli mbiu ya bango mojawapo katika Uwanja wa Tahrir mjini Cairo, Misri inayosema:

epa02820567 Egyptians are gathered at one of the Tharir square entrances as alleged thugs try to get into the square where a sit-in is taking place, Cairo, Egypt, 12 July 2011. Egypt's military rulers on 12 July warned protesters against "harming public interests" after they vowed escalation as their Cairo sit-in entered its fifth day . A spokesman for the Supreme Council of the Armed Forces, which has been running the country since February, said in a televised address that "freedom of expression is guaranteed to everyone within the limits of the law. EPA/AMEL PAIN +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kitovu cha maandamano - Uwanja wa Tahrir mjini Cairo, MisriPicha: picture alliance / dpa

" Umma usiiogope serikali yake - serikali iuogope umma wake." Likiendelea linasema:

"Watu katika nchi za Kiarabu wanataka kukomesha kabisa mtindo wa kutumia vibaya madaraka bila ya kuadhibiwa. Tunisia hapo jana ilivuna matunda ya jitahada zake za kupigania demokrasia, ilipokwenda kupiga kura kulichagua baraza la kutunga katiba ya nchi. Nchini Misri uchaguzi wa bunge utafanywa mwezi wa Novemba na Libya itakuwa na uchaguzi mwakani.

Mada ambayo haiwezi kuepukwa kabisa, ni mzozo wa madeni unaozikabili baadhi ya serikali za nchi zinazotumia sarafu ya euro. Gazeti la NORDWEST-ZEITUNG linaeleza hivi:

"Inazidi kudhihirika kuwa sarafu ya pamoja haiweza kufanya kazi, bila ya kuwepo makubaliano katika sera za uchumi na fedha. Kwa Ugiriki, huo ni ukweli uliokawia kutambuliwa. Kwa mujibu wa ripoti mpya, wataalamu wa kiuchumi wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya ECB na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, wamegudnua kuwa ifikapo mwaka 2020, nakisi ya bajeti ya Ugiriki itakuwa euro bilioni 252. Ukweli ni kuwa nchi hiyo imefilisika. Sasa hakuna njia nyingine isipokuwa kuipunguzia nchi hiyo sehemu kubwa ya madeni yake. Hata benki zitapaswa kubeba mzigo huo. Angalao katika swala hilo viongozi wa Ulaya wamekubaliana baada ya kukutana mwishoni mwa wiki iliyopita.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der franzoesische Praesident Nicolas Sarkozy (vorn, l.) unterhalten sich am Samstag (22.10.11) in einem Flur des Europaeischen Ratsgebaeudes in Bruessel auf dem Weg zu einem Treffen mit dem Praesidenten des Europaeischen Rats, dem Praesidenten der Europaeischen Kommission, dem Praesidenten der Europaeischen Zentralbank und der Direktorin des Internationalen Waehrungsfonds im Vorfeld des EU-Gipfels am Sonntag (23.10.11). Foto: Jesco Denzel/Bundesregierung/dapd
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel(kulia) na Rais Nocolas Sarkozy wa Ufaransa watofautiana juu ya njia ya kuudhibiti mzozo wa euroPicha: dapd

Gazeti la LANDESZEITUNG linasema:

"Bado kuna matumaini ya kupata ufumbuzi wa mzozo wa madeni katika kanda inayotumia sarafu ya euro, angalao hadi Jumatano, kwani Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameahidi kuwa makubaliiano yatapatikana juu ya njia ya kuudhibiti mzozo huo.

Lakini baada ya mkutano wa kilele wa kwanza mjini Brussels, kumalizika bila ya maafikiano yo yote kupatikana, gazeti hilo lina wasiwasi iwapo viongozi hao watafanikiwa kweli kuondoa tofauti zote za maoni miongoni mwao.

Mwandishi:Martin,Prema/

Mhariri:Josephat Charo