1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulinzi waimarishwa Cairo

Admin.WagnerD23 Novemba 2012

Vikosi vya usalama Misri leo vimeimarisha ulinzi mjini Cairo karibu na uwanja wa Tahrir wakati wapinzani wakipanga kufanya maandamano makubwa ya kupinga mabadiliko ya katiba yaliyoamriwa na rais Mohammed Morsi.

https://p.dw.com/p/16oZz
Egyptian anti-riot policemen and army soldiers stand alert outside the police academy courtroom as the country braces for a verdict in the trial of ousted president Hosni Mubarak in Cairo, Egypt, Saturday, June 2, 2012. The 84-year-old Mubarak, the first Arab leader to be tried by his own people, faces charges of complicity in the killing of some 900 protesters during last year's uprising that forced him from power. If convicted, he could face the death penalty. (Foto:Amr Nabil/AP/dapd)
Polisi CairoPicha: dapd

Ulinzi mkali umeimarishwa nje ya jengo la bunge, ofisi ya baraza la mawaziri na karibu na makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani wakati ambapo waandamanaji wakianza kuungana katika uwanja wa Tahrir.

Rais Morsi jana amesaini marekebisho ya katiba ambayo yanayompa kinga ya maamuzi yake kutopitiwa na mahakama. Morsi ambaye amekuwa rais wa kwanza wa Misri kuchaguliwa kiraia pia amembadilisha mwendesha mashitaka mkuu ambaye naye aliteuliwa katika utawala wa sasa uliomwondoa madarakani Hosni Mubarak.

Mamlaka mapya kwa rais

Kanuni hiyo iliyotolewa jana inalipatia kinga bunge linaloongozwa kwa wingi na chama cha kiislamu na kumpatia mamlaka mapya rais ambayo ndiyo yaliompa nguvu za kumfukuza mwendesha mashitaka mkuu na kumteua mwengine.

Mohammed Morsi, President of Egypt, addresses the 67th session of the United Nations General Assembly at U.N. headquarters, Wednesday, Sept. 26, 2012. (Foto:Jason DeCrow/AP/dapd)
Rais Mohammed Morsi wa MisriPicha: AP

Kanuni hiyo inaeleza kuwa maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na rais Morsi mpaka wakati wa uchaguzi mpya wa bunge hayapaswi kuingiliwa kisheria.

Kanuni hiyo mbali ya kuonekana kama ya kimabavu lakini pia inaelekeza kurejewa kwa mashitaka ya maafisa wa utawala

Kauli ya upinzani

Upinzani wameita amri hiyo kama ukiukwaji wa uhuru wa mahakama na kudai kwamba inamkinga Morsi ambaye tayari anao ushawishi wa mamlaka ya wabunge na nguvu za kidikteta.

Hatua hiyo ni kama inaonekana muhimu katika kulinda mapinduzi ambapo chama cha rais Morsi cha udugu wa kiislamu na washirika wenzake wamesifu amri hiyo wakisema ni ''Mageuzi'' na kuitisha maandamano makubwa hii leo kwa ajili ya kumuunga mkono rais Morsi.

Hata hivyo upo ukosoaji katika utawala wa rais Morsi ambapo wale wasiokuwa waislamu wanalalamika sauti zao kutosikika.

Katiba ni kipengele muhimu katika kipindi cha nchini Misri katika kuimarisha demokrasia. Uchaguzi wa bunge jipya hautakuwepo hadi hati hiyo itakapokamilika na kupitishwa kwa kura ya maoni maarufu.

Kanuni hiyo inatoa muda miezi miwili zaidi kwa tume kumaliza kazi yake ikimaanisha kwamba kazi ya kutengeneza rasimu inaweza ikafikia mwezi februari na hivyo kusogeza nyuma uchaguzi mpya.

Mwandishi:Sylvia Mwehozi/DPA/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman