1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulinzi Mkali Pakistan

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRV

ISLAMABAD:

Pakistan iliimarisha leo hii ulinzi katika Uwanja wake wa ndege ,ikapiga marufuku maandamano na mikutano pamoja na,uwatia nguvuni wakereketwa kadhaa wa chama cha Upinzani.Hii imefanyika siku 1 kabla kuwasili nyumbani kwa waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif kumpa changamoto jamadari Musharraf –rais wa kijeshi wa Pakistan aliempeleka Sharif kuishi uhamishoni miaka 7 iliopita.

Nawaz Sharif amepanga kuruka kesho kwa ndege kutoka London hadi Islamabad.Jamadari musharraf alimpindua Sharif hapo 1999.