1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yatafuta suluhisho mgogoro wa Iran na Marekani

Angela Mdungu
15 Julai 2019

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya, wanakutana hii leo mjini Brussels,  kujadili namna ya kuzishawishi Iran na Marekani kupunguza mvutano na kukaa katika meza ya mazungumzo

https://p.dw.com/p/3M5C5
Japan Osaka | G20 Gipfel | Emmanuel und Angela Merkel
Picha: Reuters/J. Silva

Mgogoro kati ya Iran na Marekani umezidi kufukuta tangu Raisi wa Marekani Donald Trump alipoamua kujiondoa katika makubaliano hayo ambapo Iran ilikubali kupunguza shughuli za uundaji wa silaha za nyuklia, kwa sharti la kupunguziwa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.
Kutokana na Marekani kuiwekea tena vikwazo vikali, ambavyo vinaulenga moja kwa moja mfumo wa mapato wa nchi hiyo unaotokana na mafuta, Iran imeendeleza majukumu yake ya uzalishaji wa silaha za nyukliakukiwa bado na makubaliano.

Rouhani asema Marekani imefeli
Akizungumzia mgogoro kati ya nchi yake na Marekani katika moja ya hotuba zake, Raisi wa IranHassan Rouhani amesema kuwa kila jaribio ambalo Marekani imelifanya dhidi ya Iran ndani ya miezi hii 14, liwe kwa njia za kijamii, kisiasa ama kisheria halikufanikiwa. Katika Umoja wa Mataifa kwenye mikutano mbalimbali, na uwepo wao wiki iliyopita kwenye Shirika la kimataifa la nishati na Atomiki, ambalo lilionesha kuwa hakuna hata nchi moja duniani ambayo ingesikiliza tuhuma zao.  Kando ya Marekani na baadhi ya nchi, mataifa mengine yote yaliilinda Iran.
Kutokana na msuguano huo, nchi zenye nguvu za Ulaya, Ufaransa Uingereza na Ujerumani, zimeionya Iran kuwa imeshindwa kuzingatia masharti ya makubaliano hayo. Mataifa hayo matatu, ambayo ni washirika katika makubaliano hayo  sambamba na Urusi, na China, yanatafuta namna ya kututatua mgogoro huo ambao umesababisha Marekani kuanzisha mpango unaolenga mashamblizi ya anga dhidi ya Iran, ambao Rais Trump aliusitisha katika dakika za mwisho. Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron, alimtuma mwanadiplomasia wake wa juu kwenda Iran wiki iliyopita ili kupendekeza namna ya kuituliza hali na kwamba alitaka kupitia upya maendeleo ya kidiplomasia ifikapo leo Julai 15. 

Iran Teheran - Hassan Rouhani hält Ansprache zum "Army Day"
Rais wa Iran Hassan RouhaniPicha: Getty Images/AFP

Siku ya Jumapili, Raisi Rouhani Rouhani alisisitiita msimamo wake kuwa Iran iko tayari kufanya majadiliano na Marekani, iwapo Marekani itaviondoa vikwazo ilivyovirejesha kwa Iran kuhusiana na mpango wa nyuklia. Hata hivyo Trump, hajaonesha dalili yoyote ya ya kuondoa vikwazo hivyo licha ya kujadili na Raisi wa Ufaransa  na alisema wiki iliyopita kuwa ataongeza vikwazo zaidi.