1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yashutumu uchaguzi wa bunge nchini Urusi

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWTw

MOSCOW.Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya pamoja na Baraza la Umoja wa Ulaya vimetoa taarifa ya pamoja kulaani uchaguzi wa bunge nchini Urusi vikisema hakuwa huru na haki.

Katika uchaguzi huo uliyofanyika Jumapili iliyopita Chama cha Rais Vladmir Putin cha United Russia Party kilipata ushindi mkubwa.

Ujerumani ilisema kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa kidemokrasia.

Mapema wanaharakati wa haki za binadaamu nchini Urusi, wakosaji wa serikali pamoja na wapinzani waliulaumu utawala wa Putin kwa kuuvuruga uchaguzi huo.

Chama hicho cha United Russia pamoja na tume ya uchaguzi ya Urusi vyote vimetupilia mbali shutma hizo.