1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe kusaidia kuanzisha utawala wa kisheria

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8Uv

BRUSSELS:

Umoja wa Ulaya umeidhinisha kupeleka ujumbe wa kiraia wa kama wataalamu 1,800 katika jimbo la Serbia la Kosovo.Ujumbe huo katika kipindi cha miezi minne ijayo utachukua nafasi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliopo Kosovo tangu mwaka 1999.

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya wenye polisi,wanasheria na wataalamu wa usimamizi utaisaidia Kosovo kuunda taifa lenye utawala wa kisheria.Jimbo la Kosovo linatazamiwa kujitangazia uhuru wake kutoka Serbia.Tangazo hilo linatarajiwa kutolewa siku ya Jumapili.Waziri Mkuu wa Kosovo siku ya Ijumaa aliyahakikishia makundi ya kikabila ya wachache katika jimbo hilo kuwa watu hao hawatobaguliwa baada ya Kosovo kutangaza uhuru wake.Miongoni mwa hao wachache hasa ni wakazi wenye asili ya Kiserbia.

Kwa upande mwingine,serikali ya Serbia imeonya kuwa itachukua hatua za kiuchumi na kidiplomasia kuzilipiza kisasi nchi zitakazotambua uhuru wa Kosovo.