1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa rambirambi kwa Norway

Othman, Miraji24 Julai 2011

Huku Norway ikiomboleza vifo vya si chini ya watu 92 waliouwawa katika shambulio la bomu na ufyetuliaji ovyo wa risasi, mshukiwa hasa wa hujuma hizo mbili anaripotiwa amekiri kuwa na dhamana ya visa hivyo.

https://p.dw.com/p/Rbp2
Majengo yaliyoteketezwa katika mripuko wa bomu mjini OsloPicha: dapd

Wakili wa mtu huyo, mwenye umri wa miaka 32, na anayetajwa kuwa ni Mkristo mwenye siasa za mrengo wa kulia, aliiambia televisheni ya NRK kwamba mteja wake amesema kwamba aliyapanga mashambulio hayo kwa muda mrefu.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU), aufgenommen am Montag (23.05.11) in Berlin im Konrad-Adenauer-Haus bei einer Pressekonferenz nach der Sitzung des Bundesvorstands der CDU. Die CDU wurde bei den Landtagswahlen in Bremen drittstaerkste Partei. (zu dapd-Text) Foto: Michael Gottschalk/dapd
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: dapd

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Norway na amezungumza kwa simu na waziri mkuu wa nchi hiyo, Jens Stoltenberg, kufuatia mashambuliaji yaliopteza roho za watu nchini Norway.

Nae Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amesema, Ujerumani itatoa msaada katika zoezi la uchunguzi wa kiufundi juu ya uhalifu huo na itawashughulikia waathiriwa. Amesema:

"...Ni wakati mgumu kwa Norway, lakini mimi na hakika kwamba Wa-Norway kwa umoja wao wote watayadhibiti mambo wakati huu. Wajerumani wanasimama pamoja nao na kuomboleza juu ya watu walioathirika na pia ni muhimu kwamba sisi sote hapa Ulaya, tuwe macho na kutambuwa kwamba mashambulio ya aina hiyo yanaweza pia kufanyika hapa Ulaya."

Umoja wa Ulaya umeshtushwa juu ya kile ilichokisema ni shambulio la kuchukiza katika nchi hiyo inayojulikana sana kwa juhudi zake za kutafuta amani. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Hans-Peter Friedrich, aliliaimbia gazeti la Bild am Sonntag kwamba ionekanavyo, hakuna hatari kutoka kwa watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani. Bwana Friedrich alisema, mashambulio ya kuchukiza yaliofanywa huko Norway, yanadhihirisha tena namna ya hatari ambayo watu binafsi wanaweza kuisababisha, bila ya kujali dhamira zao.