1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani ni mabingwa wapya wa mpira wa mkono

Ramadhan Ali5 Februari 2007

Kwa mara ya tatu Ujerumani ilitawazwa jana mabingwa wa dunia wa mpira wa mkono-handball baada ya kuizaba Poland mabao 29-24.

https://p.dw.com/p/CHcj
Picha: AP

Schalke ni viongozi wa Bundesliga,Taifa Stars-ya Tanzania,iko Brazil na RFonaldinho hatakuwa uwanjani kesho katika changamoto ya kirafiki baina ya Ureno na Brazil.Nigeria pia ina miadi kesho na Ghana kuamua nani ni jogoo la sdimba Afrika magharibi.

Miezi 7 tangu kumalizika kwa shangwe za Kombe la dunia la kabumbu ambamo Ujerumani ilimaliza nafasi ya 3 nyuma ya Itali na Ufaransa, Ujeruimani jana ilitawazwa mabingwa wa dunia wa mpira wa mkono-hgandball baada ya kuikomea Poland mabao 29-24 katika finali ya kusisimua ajabu kwenye ukumbi wa Kölner Arena, mjini Cologne.

Mbele ya mashabiki 19,000 waliopepea bendera za Ujerumani kama wakati wa kombe la dunia la dimba na umati mkubwa wa hadui milioni 12 usiowahi kuonekana ukiangalia katika TV,ushindi wa timu ya Ujerumani uliwakumbusha wengi shangwe za mwaka jana:

Mambo ni bambam-siamini maajabu yaliotokea hapa.

Tunataka kuiona timu bingwa,tunataka kuiona timu bingwa……..

Ubibngwa handball-mpira wa mkono ni ubingwa wa 6 kuandaliwa nchini Ujerumani mnamo miezi 9 iliopita na hii inabainisha Ujerumani ni Mecca ya michezo yenye zana za kisasa kwa maandalio ya michezo mbali mbali.

Kwa mara nyengine tena, wajerumani walionesha ulimwengu jana kwamba wao ni mashabiki wakubwa wa michezo .

Nae Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani aliipongeza timu hii ya mpira wa mkono kwa ubingwa 3 wa Ujerumani katika historia ya mashindano haya.

Ujerumani inapanga kuandaa mashindano mengine 5 ya ubingwa wa dunia mwaka huu wa 2007-mbio za baiskeli,mbio za mitumbwi,makasia,triathlon na fistball.

Alao jana ,mpira wa mkono-handball uliufunika mpira wa miguu-kabumbu hapa Ujerumani:

Katika Bundesliga-timu mpya imeparamia kileleni baada ya kitambo kirefu Werder Bremen kun’gan’gania usukani wa Ligi.

Jumamosi, mabingwa Bayern munich walichezeshwa kmindumbqwe-ndumbwe na Nüremberg mbele ya kocha wao mpya Ottmar Hitzfeld alieitwa kuliokoa jahazi linalokwenda mrama.Kwa pigo la mabao 3:0, Munich yaonesha haina lake jambo msimu huu.Lakini kileleni mwa Ligi iko Schalke 04 ambayo mara kwa mara imekuwa ikishindwa kuondoka na taji na kumalizikia makamo bingwa.Schalke lakini iliizaba Bremen 2-0 hapo jana na inadai kila kitu kina mwisho wake .Kwa ushindi huo imetoa salamu kwa Bremen kwamba huu ni mwaka wa Schalke.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza –viongozi wa Ligi-manchester United imeikomea Tottenham Hotspur mabao 4-0 kwa mabao ya christiano ronaldo ,Vidic,Scholes na Giggs.Mabingwa chelsea wako pointi 6 nyuma ya Manchester United.

Katika La Liga-Ligi ya Spian,stadi wa Kameroun, Samuel Eto’o alirejea alao kwa dakika 5 za mwisho uwanjani hatahivyo, FC Barcelona,ilishindwa kuwika mbele ya Osasuna na kumdu suluhu tu 0:0.

Nchini Ufaransa, Olympique Lyon ilikiona tena kwa mara ya tatu kile kilichomtoa kanga manyoya:Troyes ilichapa Lyon bao 1:0 na hilo likawa pigo lao la tatu katika mapambano 5 yaliopita.

Nchini Holland,PSV Eindhoven walipatwa na mkosi wao wa kwanza nyumbani walipolazwa chali na AZ AZ Alkamaar kwa mabao 3-2.Hatahivyo, Eindhoven imebakia kileleni ikiwa na pointi 56 huku mapambano 11 yakisalia kumaliza msimu.

Katika SERIE A-Ligi ya Itali, maji yalizidi unga mwishoni mwa wiki.Fujo lilitanda uwanjani na mitaani na chama cha mpira kikaamua kusimamisha Ligi wakati huu.Askari mmoja polisi aliuwawa na mwengine kujeruhiwa vibaya.

Waziri wa michezo wa Itali, Giovanna Melandri aliahidi hapo jana kuwa, hatua barabara zitachukuliwa tena haraka kumpunga shetani wa dimba nchini Itali na kuwazima wahuni wanaozusha fujo viwanjani.

Mashabiki wa dimba nchini na nje yake wanasubiri.

Taifa Stars timu ya taifa ya Tanzania imefunga safari ya Brazil anakotoka kocha wake Masimo kujinoa kwa miadi yake ya mwezi ujao na Senegal.

Kesho kuna changamoto kadhaa za kirafiki:

Brazil,ina miadi kesho na Ureno inayoongozwa na kocha wao wa zamani Luis Felipe Scolari.Ureno iliilaza Brazil mabao 2:1 Machi,2003 na Brazil chini ya kocha Dunga ,inataka kesho kulipiza kisasi.

Lakini, inabidi kuteremka uwanjani bila Ronaldinho alieumia.Kinyume chake Cristiano Ronaldo wa Ureno,hivi sasa amekuwa hatari sana na mkuki wake waweza kuichoma Brazil hapo kesho.

Kesho pia –asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mahasimu 2 jirani-Ghana na Nigeria wanakutana nje ya London kufufua uhasama wao wa kale wa dimba na kujibu swali:nani hasa mbabe wa kabumbu Afrika Magharibi.Mpambano huo huko London utachezwa huku Nigeria ikiwa kwa mara ya kwanza chini ya kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani Berti Viogts.

Nigeria pia haikushindwa na Ghana tangu 1992 na ndio ilio kileleni mwa orodha ya FIFA miongoni mwa timu bora za Afrika wakati huu.Ghana lakini, ilitamba katika Kombe lililopita la dunia hapa Ujerumani ambamo ilicheza duru ya pili wakati nigeria,ilibaki nyumbani.

Muakilishi mwengine wa Afrika katika Kombe la dunia hapa Ujerumani-Angola imeikasirikia mno Senegal kuvunja miadi yao ya kukutana uwanjani wiki ijayo.Senegal imeamua kwenda Ufaransa badala ya Angola kucheza dimba.