Ujerumani na Uingereza leo Wembley | Michezo | DW | 22.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ujerumani na Uingereza leo Wembley

Zinapokutana Ujerumani na Uingereza katika medani ya dimba,mtu haachi kukumbuka ile finali ya kombe la dunia katika uwanja huo 1966 na lile bao la kutatanisha la Uingereza-liliingia au la.

Katika marudio ya finali ya kombe la dunia 1966,Uingereza inacheza jioni hii na Ujerumani katika uwanja mpya wa Wembley.Timu zote mbili zina wachezaji wanaougua-Ujerumani inateremka bila ya mkuki wake Miroslav Klose na nahodha Michael ballack wakati Uingereza bila ya mzinga wake Wayne Rooney na Steven Gerrard.

Brazil pia inaingia uwanjani huko Montpelliar,Ufaransa kucheza na Algeria huku kaka na Ronaldinho wakiwa wachezaji wa akiba tu.

Tukianza na changamoto ambayo huwezi kuieleza ni ya kirafiki tu kati ya England na Ujerumani uwanjani Wembley, wenyeji England wamemuita nahodha wao wa zamani David Beckham kuliokoa jahzi lisiende mrama.Na hasa kwa kuwa mastadi kama Steve Gerrard,Wayne Rooney na Owen Hargreaves na hata Andy Johnson wa Everton hawatakuwa uwanjani.

Lakini David Beckham ni fit kucheza leo au kocha Steve McClaren anamchezesha tu ?

Hili ni jibu lake:

“Tulisema tokea mwanzo David aliporejea katika timu kuwa itategemea mchezo wake.Amerudi katika kikosi hiki kutokana na mchezo wake na atachezeshwa kwa muujibu wa mchezo wake.”

Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amemualika kocha wa zamani wa Ujerumani, Jürgen Klinsmann kuwa nae uwanjani Wembley.Je, anahitaji tipu fulani kutoka kwa Klinsmann na kutocheza kwa nahodha wake Ballack na mshambulizi Miroslav Klose kutaathiri vipi uwezo wa Ujerumani ? Tusubiri tuone.

Je, nani ataondoka na ushiundi leo ?

Mpambano mwengine unaokodolewa macho jioni hii ni ule unaochezwa upande wapili wa mpaka-huko Montpelliar,Ufaransa kati ya Algeria na Brazil.

Brazil imeamua kwanza kuwaweka ubaoni akina Ronaldo na Kaka:

Simba wa nyika Kamerun wana miadi leo na Japan

Mjini Tokyo.Na stadi wao Samuel Eto’o amejiunga nao.

Katika changamoto ya jana usiku wenyeji wa kombe lijalo la Afrika la Mataifa-Ghana walitoka suluhu ya bao 1:1 na Senegal.Hatahivyo, kocha wa Ghana Claude Le Roy, anaaminikuwa timu yake ndio itakayotwaa kombe la Afrika la mataifa mradi tu staid wao Michael Essien atakuwa fit.

Mwishoe, mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni yakinyemelea kuanza mjini Osakas,Japan mwishoni mwa wiki,msenegal Lamine Diack, amechaguliwa tena jana kwa kipindi cha mwisho cha miaka 4 kama rais wa IAAF-shirikisho la riadha ulimwenguni.

 • Tarehe 22.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbE
 • Tarehe 22.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbE