1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na kutaifisha benki

18 Februari 2009

Serikali ya Ujerumani imepitisha leo sheria ya kutaifisha:

https://p.dw.com/p/Gwqo
Chancellor Angela Merkel na Sarkozy.Picha: AP

Serikali ya Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, imepitisha leo mswada wa sheria kuweza kutaifisha banki zozote nchini zilizokumbwa na msukosuko wa fedha -hatua ambayo ikionekana mwiko kunyakua mali ya mtu tangu kumalizika vita vya pili vya dunia.Ikiepuka kuigiza utawala wa Manazi ulionyakua mali za wayahudi .

Sheria hii sasa huenda ikaongoza kutaifishwa kwa Benki ya mikopo ya majumba-Hypo Real Estate inayopepesuka.

Katika kuweka kando ahadi iliotoa baada ya vita vya pili vya dunia ya kuheshimu mali za mtu binafsi na kutotaifisha,Ujerumani imekuwa serikali nyengine kuachana na miko hiyo ya soko huru na kutumia akiba za fedha za serikali kuyaokoa mabenki ya kibinafsi yanayoregarega.

Mhanga wa kwanza yamkini likawa Banki la mikopo ya majumba la kusini mwa ujerumani-HYPO REAL ESTATE.

Nchi nyengine pamoja nazo Uingereza na Jamhuri ya Ireland,tayari zimeshataifisha baadhi ya mabanki yao zikitoa hoja ya jinsi msukosuko wa fedha ulivyo mkubwa na haja iliopo kuwalinda walipakodi.

Hatahivyo, Ujerumani ikiona taabu sana kufuata mfano huo wa kile inachokiita "Enteignung"-kutaifisha mali ya watiahisa-shareholders- kwani ni mzigo kichwani mwake ikikumbuka hali ilivyokuwa wakati wa utawala wa Manazi nchini Ujerumani pale mali za wayahudi ziliponyakuliwa kwa nguvu mnamo miaka ya 1930.Hali sawa na hiyo ilikuwapo katika ile iliokua Ujerumani ya Mashariki (GDR) baada ya vita vya pili vya dunia pale mali za baadhi ya watu binafsi zilitaifishwa.

Kanzela Angela Merkel akiitetea hatua ya leo alisema:

"Tumechukua hatua hii sio kuudhofisha mfumo wa soko huru,ni upuuzi kudai hivyo, bali tumefanya hivyo, ili kuufanya uchumi wa soko huru kurejea kufanya kazi barabara.

Na ili kuzitumia fedha za walipa kodi inavyopasa,imetubidi sasa kuona tunajipatia wingi wa sauti mfano katika Hypo Real Estate Bank."

Hatua hizi mbali mbali zilizochukuliwa na serikali zimeshindwa hadi sasa kuleta nafuu katika masoko ya fedha.Hisa katika masoko ya dunia kwa muujibu zilivyopimwa na shirika la MSCI ziliteremka chini leo hivyo zikimurika kuporomoka mno jana usiku barani Asia.

Jana Rais Barack Obama wa Marekani alitia saini kuidhinisha kuwa sheria matumizi ya kitita cha dala bilioni 787 tangu kuwapunguzia wananchi kodi hadi kukuza ajira-hatua kubwa kabisa ya aina hii katika historia ya Marekani.

Rais Obama akasema mpango huo wa kuustawisha na kuimarisha uchumi ndio "mwanzo wa mwisho wa msukosuko wa sasa".

Lakini matatizo 2 pacha yakichomoza kila mara kuanguka kwa bei za vitu na shida ya kupata mikopo,masoko ya fedha yamo katika wasi wasi bado kuhusu hali ya siku zijazo.

Kimsingi, katiba ya Ujerumani au (Grundgesetz) inakataza mtindo wa kutaifisha mali ya mtu binafsi bila ya kwanza kutunga sheria mpya.hatua ambayo imechukuliwa leo.katika kisa cha Benki ya majumba ya Hypo Real Estate, serikali ya Ujerumani imechagua bora kulitaifisha benki hili kwavile inahisi bila kufanya hivyo,inaweza kujikuta shidani kulidhibiti kabisa mikononi mwake.Sababu ni kuwa mtiaji raslimali wake mmoja ni JC Flowers wa Marekani mwenye kumiliki robo ya hisa katika Banki hiyo ya Hypo Real Estate.

Kwahivyo, serikali ya ujerumani itaendelea kupatana na JC Flowers na mazungumzo yao yakishindwa, serikali ya Ujerumani itajaribu kulimiliki kabisa banki hilo kwa kutia raslimali yake kubwa zaidi wakati wa mkutano wa wenyehisa katika Banki hiyo.Sheria hii mpya iliopitishwa leo na baraza la mawaziri mjini Berlin,inawezesha hatua hiyo.