1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani leo kumpata rais mpya

30 Juni 2010

Rais mpya wa Ujerumani anachaguliwa , leo na baraza maalumu la shirikisho lenye wajumbe 1244.

https://p.dw.com/p/O6No
Mgombea urais wa Ujerumani kwa tiketi ya CDU/FDP Christian WulffPicha: picture-alliance/ dpa

Atakaechaguliwa leo atachukua nafasi ya rais wa hapo awali, Horst Köhler, aliejiuzulu mwezi uliopita.

Wanagombea wadhifa huo ni waziri mkuu wa sasa wa jimbo la Lower Saxony, Chrsitian Wullf, na aliekuwa anasimamia idara kuu ya nyaraka za siri za idara ya ujasusi wa ndani ya Ujerumani Masharrikiya hapo awali, Bwana Joachim Gauck, mwenye umri wa miaka 70.

Waziri Mkuu Christiana Wullf ni mjumbe wa vyama vya serikali ya mseto na CDU na chama cha Waliberali, FDP. Vyama hivyo kwa pamoja na chama ndugu cha CSU vitawapeleka wajaumbe 644 yaani 21 zaidi ya wingi unaohitajika ili mjumbe wao ashinde .

Mgombea mwingine, Joachim Gauck, ni mgombea anaeungwa mkono na vyama vya upinzani-SDP na chama cha kijani. Kwa pamoja vyama hivyo vitawapeleka wajumbe 462.

Lakini Gauck mwenyewe hayumo katika chama chochote .

Kwa hiyo, hesabu zinaonyesha kwamba mgombea wa vyama vya serikali anatarajiwa kupita katika kinyang'anyiro cha leo.

Wagombe hao ni watu wanaotofautiana kwa namna nyingi .

Kwanza kabisa mgombea wa vyama vinavyoongoza serikali, Christian Wullf, amekulia katika upande wa Magharibi wa Ujerumani. Mgombea wa vyama vya upinzani, Joachim Gauck, alikuwa mwanaharakati wa kupigania uhuru katika sehemu ambayo hapo zamani ilikuwa inaitwa Ujerumani ya mashariki.

Juu ya hayo mgombea huyo amesema:

Der Präsidentschaftskandidat Joachim Gauck
Joachim Gauck,Picha: picture-alliance/dpa

"Tulikuwa Mashariki kwa sababu tulilazimishwa .Lakini katika fikira zetu tulikuwa na wazo la uhuru ambao haukuwapo katika upande wa Mashariki, lakini ulistawi katika Magharibi."

Joachim Gauck, asiyekuwa na chama chochote, hana matatizo na wahafidhina na Waliberali. Kwani angeliweza kuwa mgombea wa vyama vya serikali na vyama vya upinzani kadhalika.

Vyama vya upinzani vilimpendekeza Gauck. Kansela wa Ujerumani alipewa taarifa lakini alilikataa pendekezo hilo japo anamthamini sana Bwana Gauck.

Mgombe mwingine Christian Wullf aliependekezwa na vyama vinavyoingoza serikali . Christian Wullf alianza kuvuta pumzi ya uhuru tokea siku ya kwanza alipozaliwa katika Ujerumani magharibi.

Wullf mwenyewe anasema.

´´Muhimu ni kwamba natoka katika nasaba ya kati na nadhamiria kubakia katika nasaba hiyo. Kwangu ni jambo la kuvutia ikiwa rais atakaefuatia atakuwa mtu anaetoka katika rika la kati. Mtu mwenye uzoefu wa kuleta pamoja kazi na majukumu ya familia´´.

Christiana Wullf ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa leo kuwa rais mpya wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani.

Amesema akichaguliwa ataendeleza sera za Horst Köhler, rais wa hapo awali alieliweka bara la afrika moyoni.

Köhler alizetembelea nchi kadhaa za Afrika kuhudhuria vikao na ushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mwanasiasaa huyo amesema kwake ni wazi kabisa kwamba Ujerumani inapaswa kuuendeleza uhusiano na Afrika ulioanzishwa na rais wa hapo awali-

Mwandishi/ Martin Beutler/ZAR/

Tafsiri/Mtullya abdu/

Mhariri:Miraji Othman