Ujerumani imeyaaga mashindano ya kombe la dunia ya wanawake | Michezo | DW | 10.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ujerumani imeyaaga mashindano ya kombe la dunia ya wanawake

Timu ya taifa ya wanawake ya Japan imeifunga timu bingwa mtetezi Ujerumani 1-0 katika robo fainali za mashindano ya kombe la dunia ya wanawake mjini Wolfsburg

default

Kerstin Garefrekes wa timu ya Ujerumani apigwa na mshangao baada ya bao la Japan

Katika mashindano yanayoendelea ya Kombe la Dunia la wanawake, mabingwa watetezi Ujerumani, wametolewa kwenye mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Japan kunako dakika 120 ya mchezo huo.

Frauen-Fußball-WM Japan - Neuseeland Japan's Yuki Nagasato Tor

Wavu ulitikisika kwa kishindo cha Mpira

Ushindi wa Japan mjini Wolfsburg umezima matumaini ya Ujerumani kujinyakulia mara ya tatu mtawalia, taji la mashindano haya.

Wakati huo huo, Japan imefuzu kwenye nusu fainali za mahsindano hayo na inatarajiwa kupambana na Sweden au Australia.

Frauen-Fußball-WM 2011 Viertelfinale Deutschland - Japan

Sherehe kwa Japan

Mapema hapo jana, Ufaransa iliifunga timu ya Uingereza kupitia mikwaju ya penalti mjini Leverkusen na pia kufanikiwa kuingia kwenye nusu fainali hizo. Ufaransa sasa itakabiliana na Marekani au Brazil.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Dpae/Zdf
Mhariri:Martin,Prema

DW inapendekeza

 • Tarehe 10.07.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11sNo
 • Tarehe 10.07.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11sNo