1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haijafanya vya kutosha Rio

Admin.WagnerD19 Agosti 2016

Hayajakuwa mashindano mazuri ya Olimpiki kwa Ujerumani katika michezo mingi, lakini ina matumaini ya medali ya dhahabu katika soka, wakati chama cha riadha nchini Marekani kimeomba radhi kwa tabia ya waogeleaji wake.

https://p.dw.com/p/1Jltg
Brasilien Olympische Spiele Rio 2016 - Kugelstoßen - David Storl, Deutschland
Mchezaji wa kurusha tufe David Stort wa UjerumaniPicha: Reuters/D. Ebenbichler

Maafisa wa ngazi ya juu wa Ujerumani wako katika mbinyo mkali kuchukua hatua baada ya kuporomoka kwa ushindi wa taifa hilo katika olimpiki mjini Rio de Janeiro.

Kwa kile kinachoonekana sasa kuwa mavuno hafifu sana ya medali kwa timu ya Olimpiki ya Ujerumani tangu nchi mbili za Ujerumani kuungana mwaka 1990, hali hiyo inasababisha rais wa chama cha michezo ya Olimpiki nchini Ujerumani DOSN Alfons Hoermann kuhofia hali ya baadaye.

PK DOSB
Rais wa chama cha wanamichezo wa Olimpiki nchini Ujerumani Alfons Hoermann(kushoto)Picha: picture-alliance/dpa

Iwapo hatutachukua hatua za haraka na za wazi na kuwa na ujasiri wa kubadilisha mambo, mashindano ya olimpiki ya mjini Tokyo mwaka 2020 na yale ya 2024 na 2028 hayatakuwa kama tunavyofikiria," alisema Hoermann.

Medali nyingi kutoka Rio kuliko Ujerumani ilivyopata mjini London katika michezo ya gymnastic , mpira wa mikono katika ufukwe na mbio za ndani za baisikeli haziwezi kuficha ukweli kwamba Ujerumani imepoteza uwezo wake miongoni mwa wanamichezo bora duniani katika michezo mingi.

Kashfa ya waogeleaji

Wakati huo huo waogeleaji wawili wa Marekani walirejea nyumbani kutoka Brazil siku ya Alhamis huku mashabiki wa Brazil wakiwazomea , wakiwaita waongo, na wasio wakweli, naq polisi wamewashutumu kwa kutengeneza stori juu ya kuporwa na majambazi wenye silaha katika michezo hiyo ya olimpiki.

USA Omaha Schwimmer Jimmy Feigen (Ausschnitt)
Muogeleaji Jimmy Feigen wa MarekaniPicha: picture-alliance/AP Photo/M. J. Terrill

Kamati ya olimpiki ya Marekani USOC iliomba radhi baada ya kuondoka kwa Gunnar Bentz na Jack Conger , ambao ni miongoni mwa waogeleaji wanne wa Marekani walionekana kuwa walidanganya juu ya kusimamishwa kwao na polisi waliokuwa na silaha mapema siku ya Jumapili na kuporwa.

Mwenda mbio mahiri duniani

Hata hivyo tukio hilo lililainishwa na ushindi wa mwanariadha mahiri wa Jamaica Usain Bolt ambaye alishinda medali yake ya pili ya dhahabu katika mashindano haya, na anawania sasa medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 mara nne kupokezana vijiti. Bolt na wenzake wa jamaica walishinda medali ya dhahabu mjini Beijing na London , ambako timu hiyo iliweka rekodi ya dunia.

Rio 2016 Olympia Leichtathletik Usain Bolt posiert nach 200 m Rennen
UsainBolt wa JamaicaPicha: picture-alliance/Zumapress/Li Ming

Bolt alisema haya yatakuwa mashindano yake ya mwisho ya olimpiki, lakini muogeleaji wa Marekani Michael Phelps alisema hivyo, lakini alirejea tena katika mashindano haya na kunyakua medali kadhaa.

DFB Pokal

Kwa upande wa kandanda, mashindano ya kombe la shirikisho DFB Pokal nchini Ujerumani yanaendelea leo ambapo timu za daraja la kwanza za FC Kolon, Schalke 04, Borussia Moenchengladbach, na Wolfsburg zitajitupa uwanjani katika duru ya kwanza ya kombe hilo msimu huu.

Ligi ya Uhispania La Liga inaendelea tena leo ambapo mabingwa watetezi FC Barcelona iko nyumbani ikiisubiri Betis Sevilla, Villareal inakwenda nyumbani kwa Granada wakati Sevilla inaikaribisha Espanyol Barcelona.

Fussball 1.Bundesliga, FC Bayern München - Hannover 96, Pep Guardiola wird verabschiedet Muenchen
Kocha wa manchester City Pep GuardiolaPicha: Imago

Jumapili ni zamu ya mabingwa wa Ulaya Real Madrid ikiumana na Real Sociedad na Atletico Madrid ina miadi na Alaves.

Jürgen Klopp Liverpool UEFA Liverpool FC vs Sevilla FC
Kocha wa Liverpool Juergen KloppPicha: Getty Images/J.Soriano

Katika Premier League nchini Uingereza Mabingwa watetezi wana kibarua na Arsenal iliyojeruhiwa wiki iliyopita na Liverpool , wakati Man City inasafiri hadi Stoke City kuwania pointi tatu nyingine na kuhakikisha kocha mpya Pep Guardiola anaanza vizuri msimu wake wa kwanza nchini Uingereza.

Burnley wanakikaribisha kikosi cha kocha Juergen Klopp cha Liverpool, na Watford wako nyumbani wakiisubiri Chelsea ya kocha Antonio Conte.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae /ape

Mhariri: Josephat Charo