1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru wa vyombo vya habari wakabiliwa na mtihani

8 Desemba 2010

Kesi ya Assange ni kitisho kwa uhuru wa vyombo vya habari

https://p.dw.com/p/QTGG
Muasisi wa tovuti ya WikiLeaks, Julian AssangePicha: AP

Baada ya wiki kadhaa za vuta nikuvute, muanzilishi wa Wikileaks Julian Assange amejisalimisha kwa polisi ya Uingereza. Bwana Assange anakabiliwa hasa na tuhuma za ubakaji nchini Sweden. Inasemekana pia kua Marekani ingependa kukapidhiwa Bwana Assange ili afikishwe mbele ya mahakama ya nchi hio, kwa mashtaka ya ujasusi.

Habari muhimu na za siri zinazotangazwa na mtandao wa Wikileaks zinavyoenea haraka, ndivyo shida za kibinafsi za muanzilishi wa Wikileaks, Bwana Julian Assange, raia wa Australia zinavyoelekea kua mzozo wa kisiasa wa kimataifa.

Hakuna anaejua kikamilifu, nini kilichotokea usiku wa siku hizi mbili za mwezi ogosti nchini Seeden; zinazohusishwa na tuhuma dhidi ya Bwana Assange.

Lakini inaelekea ofisi ya mwendesha mashtaka wa nchi hio haikuweza kuelewa kivingine mazingira ya shida zinazomkabili Bwana Assange, kama si mkono wa serikali ya Marekani dhidi ya Wikileaks.

Kwa taifa kubwa kama Marekani, taarifa za Wikileaks zimekua tukio lililoikera sana na haijafurahia kushuhudia, vipi kundi dogo tu lilivyozifichua siri zake muhimu kwa dunia nzima, bila kujua ifanye nini.

Ilianzia shida za Marekani katika vita vyake vya Afganistan, ikaja mikasa ya vita vya Irak, na hatimae ujumbe mbali mbali wa kidiplomasia baina ya maafisa wa wizara ya mambo ya kigeni wa Marekani.

Taarifa za wikileaks zimeathiri sura ya Marekani katika nchi za nje. Lakini, ni kipya ambacho mtu alikisoma katika habari hizo za Wikileaks kuhusu Afganistan ambacho kilikua hakijulikani tangu zamani? Nini ambacho wataalamu wa Afganistan walikua hawajasema. Kuna chochote kipya ambacho kinatupatia nafasi ya kukosoa mtazamo wetu kuhusu vita vya Irak?

Bila shaka ni jambo la kuchukiza, kwamba maafisa wa kidiplomasia wa Marekani wamejikuta katika hali ambayo wanabidi kuomba msamaha kwa kuhusika na ujumbe uliosababisha madhara. Lakini je, madhara gani.

Madhara yanaweza kuzungumzwa kwa mfano, wakati ambapo Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton, katika ujumbe uliopewa jina la "Cablegate" anapodai kuwepo "hujuma dhidi ya jumuia ya kimataifa". Au wakati ambapo Bwana Assange anapotuhumiwa kua msaliti, gaidi na muhalifu mkubwa.

Madhara yanakuwepo wakati mtandao wa kulipia wa Paypal Wikileaks unapokuwea huwezi kutumiwa, Kadi za benki za kulipia zinakuwa haziwezi kutumiwa, au wakati mfumo mzima wa malipo kwa kutumia Amazon Wikileaks unapofutwa.

Kwa vyovyote vile, uhuru wa maoni unalindwa na mahakama kuu ya Marekani, na umefafanuliwa zaidi hata kuliko ilivyo hapa Ujerumani. Lakini sasa swali hili kuhusu uhuru wa maoni nchini Marekani, linaulizwa pia katika mitandao ya Internet nchini China, kwamba kwa umbali gani kuna uhuru wa maoni nchini Marekani?