1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Ugonjwa usiojulikana wazuka Uganda

Maradhi yasiyojulikana yaligunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita katikati mwa Uganda

Uganda inashirikiana na wataalamu wa afya wa kimataifa kutambua kiini cha maradhi yaliyosababisha vifo vya 38 kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, maradhi hayo yasiyojulikana, yaligundulika kwa mara ya kwanza tarehe 10 mwezi uliopita, katika wilaya kadhaa kwenye neo la kati huko kaskazini mwa Uganda.

Vyombo vya habari vya ndani na vile vya kimataifa vimeyaelezea maradhi hayo kuwa ni ugonjwa wa tauni, ambao mara ya mwisho kuikumba Uganda ilikuwa mwaka 2008.Wizara ya afya ya Uganda imesema kuwa dawa zimepelekwa kwenye eneo ambapo zimesaidia kuzuia kuendelea kutokea kwa vifo zaidi.

 • Tarehe 08.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QTJM
 • Tarehe 08.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QTJM