1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda: Watu wengi wahofiwa kufariki kutokana na maporomoko ya ardhi

26 Juni 2012

Huko Mashariki mwa Uganda ambapo idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliotokea jana (25.06.2012) imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 100, huku wengine wengi wakiwa hawajulikani waliko.

https://p.dw.com/p/15LPu
Wananchi wakijaribu kuwaokoa watu waliofunikwa na udongo
Wananchi wakijaribu kuwaokoa watu waliofunikwa na udongoPicha: AP

Kwa sasa shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo hilo, huku kukiwa na changamoto kubwa kufuatia matope mazito yaliozunguka eneo hilo.

Amina Abubakar amezungumza na mwandishi habari aliye katika eneo hilo kwa sasa, David Sekeka, na mwanzo anatuambia hali halisi ya mambo yalivyo kwa sasa.

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri Othman Miraji.