1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yakosolewa vikali na Umoja wa Ulaya

15 Septemba 2010

Imechukua muda mrefu lakini hatimae Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya imeeleza msimamo wake kuhusu hatua zilizochukuliwa na Ufaransa kuwafukuza Waroma nchini humo.

https://p.dw.com/p/PD2b
Viviane Reding, Vizepräsidentin der EU-Kommission im Brüsseler Büro, 9.9.2010.
Viviane Reding,mkuu wa masuala ya sheria katika Umoja wa Ulaya.Picha: DW

Halmashauri hiyo isikubali kupuuzwa na Ufaransa.Waroma pia ni wakaazi wa Umoja wa Ulaya na wana haki zao.

"Ni aibu. Nilidhani kuwa kufuatia Vita Vikuu vya Pili, Ulaya haitoshuhudia tena tukio kama hilo. Sasa inatosha kabisa."

Hayo alitamka kwa hasira Viviane Reding, mkuu wa masuala ya sheria wa Umoja wa Ulaya, huku akigonga mkono mezani. Hata ikiwa raia huyo wa Luxembourg hukasirika mara kwa mara, hayo ni maneno makali aliyotumia kuhusu vile Ufaransa ilivyowatendea Waroma. Lakini safari hii, kamishna huyo wa sheria ana kila sababu ya kukasirika.

Kwani tangu miezi kadhaa,serikali ya Ufaransa imefanya kila iwezacho kuwafukuza wahamiaji wa Kiroma waliotokea Rumania na Bulgaria. Zoezi hilo kubwa lilifanywa kwa ukatili usio na mfano. Wakaazi wa Umoja wa Ulaya wana haki ya kujiamulia wapi wanakotaka kuishi ndani ya umoja huo, bila ya kujali asili yao. Kwa hivyo, amri iliyotolewa na maafisa wa Kifaransa kubomoa kambi na hasa zile za Waroma, ni ubaguzi wa kikabila. Licha ya mawaziri wawili kukanusha tuhuma hizo,ni dhahiri kuwa hatua hazikuchukuliwa kufuatia uchunguzi wa kesi moja moja, bali jamii nzima ya Waroma ndio iliyolengwa.

Kwa hivyo, hapo Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya haikuwa na budi kuingilia kati, kwani ni wajibu wake kufanya hivyo kama mlinzi wa mikataba ya umoja huo. Na Ufaransa si mwanachama yo yote tu bali ni miongoni mwa wanachama muhimu kabisa na mmojawapo wa waasisi wa jumuiya ya Ulaya kama Umoja wa Ulaya ulivyokuwa ukijulikana hapo mwanzoni.

European Commission President, Jose Manuel Barroso addresses reporters during a news conference after his reelection at the European Parliament in Strasbourg, eastern France, Wednesday, Sept. 16, 2009. The European Parliament gave Barroso another five-year term as European Commission president Wednesday, but its vote reflected lingering misgivings about the conservative ex-Portuguese premier in the EU assembly. (AP Photo/Christian Lutz
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso.Picha: AP

Kwa kweli, halmashauri hiyo ingechukua hatua mapema zaidi. Labda haikufanya hivyo kwa sababu ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso. Yeye hujaribu kujiepusha na mzozo wo wote ule na serikali - hasa inayotoka kambi yake ya kihafidhina.

Alichofanya Viviane Reding ni sahihi. Iwapo Ufaransa itashtakiwa na halmashauri hiyo kuwa imekiuka sheria za umoja huo, sasa si muhimu hivyo. Heba ya serikali ya Rais Sarkozy imeshaingia dosari ya kutosha.

Mwandishi: Ahrens,Sylivie/ZPR

Mpitiaji: M.Abdul-Rahman