1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchunguzi wa PISA kuhusu kiwango cha elimu duniani

Oumilkher Hamidou8 Desemba 2010

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu ya taasisi ya uchunguzi ya PISA Ujerumani yafanya vyema katika sekta ya elimu ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

https://p.dw.com/p/QT2V
Waziri wa elimu wa serikali kuu bibi Annette Schavan(kulia) akionyesha ripoti ya mwaka huu ya PISAPicha: picture alliance/dpa

Mada mbili zimehanikiza magazetini hii leo: uchunguzi uliofanywa na taasisi ya jumuia ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD inayoshughulikia masuala ya elimu ulimwenguni-PISA na kuwekwa kizimbani muanzilishii wa tovuti ya Wikileaks Julian Assange.

Tuanze lakini na uchunguzi wa taasisi ya Pisa unaonyesha Ujerumani imefanya vizuri ikilinganishwa na miaka iliyopita.Hata hivyo gazeti la "Rhein-Zeitung" linajiuliza:"Ndo kusema watu waridhike na matokeo hayo tu au bado kuna mengi ya kufanya?Hata wale wenye kushuku wanakiri kwamba mengi yametendeka tangu Ujerumani ilipoungana upya.Viwango vya aina moja vya elimu vimewekwa kote nchini Ujerumani.Mfumo wa watoto kubakia siku nzima shuleni umepata ridhaa takriban ya vyama vyote vya kisiasa hivi sasa.Na kwamba shule za chekechea haziangaliwi tena kuwa ni mahala pa kuwatunza watoto tuu ,bali mahala muhimu pa kuwapatia mafunzo watoto tangu udogoni mwao,nalo pia ni suala lililowaingia watu akilini hata katika majimbo ya magharibi.Mkondo huu mpya wa kutia moyo isiwe sabababu lakini ya kuringa.Licha ya dalili za kutia moyo ambazo hakuna anaeweza kuzibisha,bado kiwango cha elimu cha watoto nchini Ujerumani kinategemea posho la wazee wao likoje.

Gazeti la "Augsburger Allgemeine" linaandika:"PISA imesaidia pakubwa hata kama bado kuna mengi ya kufanywa ili kuuimarisha mfumo wa elimu humu nchini.Watoto wetu siku za mbele watalazimika kushindana katika soko la ajira la kimataifa pamoja na watoto hodari kutoka China na Korea ya kusini.Huko watoto wanahimizwa tangu wakiwa shuleni.Lakini nchi hizo zisichuzkuliwe kua ni mfano wa kuigizwa badala yake elimu tuu ndio tunayobidi kuiangalia kuwa ni kitu cha thamani."

Assange Festnahme 2010 London NO FLASH
Gari linalosewmekana ndilo lilimsafirisha Julian Assange kumpeleka kizuwizini mjini LondonPicha: AP

Mada yetu ya pili magazetini inahusu kujisalimisha muanzilishi wa tovuti ya Wikilweaks kwa polisi nchini Uengereza.Gazeti la "Badische Zeitung" linaandika:"Tuhuma dhidi ya mwanaharakati wa mtandao zinahusu mambo yaliyotokea Agosti.Yadhihirika lakini kana kwamba mambo hayo hayakuwa bayana vya kutosha kuweza kukamatwa tangu wakati huo .Lakini pia hayakuwa mepesi kuweza kusahauliwa.Yote haya lakini hayastahiki kuwa na mafungamano hata akidogo na kasheshe ya kufichuliwa nyaraka za siri za Marekani.Hata hivyo mambo mhayo mawili hayawezi kutenganishwa.Wakulaumiwa hapo ni kila mmoja:mashabiki na wakosoaji wa Assange.

Nalo gazeti la "Südkurier" linaandika:"Julian Assange,muanzilishi wa tovuti ya Wikileaks amejisalimisha kwa polisi-ni uamuzi wa busara alioupitisha.Kwasababu hivi sasa ni jukumu la mahakama kudhihirisha makosa aliyofanya.Hatuhumiwi kufichua siri-hasha,anatuhumiwa kuhusika na ubakaji.Sasa kwanini akawa anasakwa kwa udi na ambari kama vile?Hali hiyo inawafanya wanamtandao wafikirie dhana za kila aina.Ukweli ni kwamba Julian Assange alikuwa akipendwa wakati wote ule ambao alikua akifichua siri za waimla wa dunia hii.Lakini safari hii amejitafutia mashaka kwa kujaribu kushindana na dola kuu Marekani.Dola linaloheshimu sheria halijali visa kama hivyo.Jibu lake kwa visa kama hivyo ni kesi ya haki.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Mpitiaji:Abdul-Rahman Mohamed