1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa dunia kushuka kwa 3%

23 Aprili 2009

Wakati mawaziri wa fedha wa nchi Saba tajiri na kutoka nchi 20 zinazoendelea wanajiandaa kwa mkutano mjini Washington, shirika la fedha la kimataifa IMF limetoa utabiri unaonesha kuwa uchumi wa dunia utashuka

https://p.dw.com/p/HcZA
Nembo ya IMF na pesaPicha: AP/ DW-Fotomontage




Siyo ripoti ya kufurahisha hata kidogo!

Shirika hilo limetabiri kuwa uchumi wa dunia utanywea sana mnamo mwaka huu na athari za mgogoro wa fedha zitaendelea kung'wengenya ' zaidi kuliko ilivyotarajiwa hapo awali.

Shirika la fedha la kimataifa IMF limebashiri kuwa uchumi wa dunia utashuka kwa asilimia 1.3 mnamo mwaka huu.

Katika ripoti yake ya kipindi cha nusu mwaka juu ya hali ya uchumi wa dunia, taasisi hiyo imesema kuwa uchumi huo umedorora kwa kiwango kikubwa kutokana na mgogoro wa fedha na kutokana na kupotea kwa ima ni.

IMF imeeleza kwamba uchumi wa dunia unaseserekea katika mdodoro wa kina kisichokuwa na kifani tokea kumalizika vita kuu vya pili na hali y a siku za usoni bado ni tashwishi- yaani wasiwasi mkubwa.

Hii ni mara ya tatu kwa shirika la fedha la kimataifa IMF kujirekebishakatika utabiri wake, mwelekeo ukiwa ni wa kushuka chini.

Mapema mwezi januari shirika hilo lilitabiri ustawi wa asilimia 0 nukta 5 lakidi kufikia mwezi machi lilitoa makisio ya kushuka kwa uchumi kati ya asilimia 0nukta tano hadi asilimia 1.

Nchi za viwanda ndizo hasa zitakazoathirika zaidi. Shirika la IMF llimebashiri kunywea kwa pato jumla la ndani kwa asilimia 3,nukta 8 mnamo mwaka huu.

Uchumi wa Marekani utanywea kwa asilimia 2 nukta nane wakati uchumi wa Japan utashukaa kwa asilimia 6.2.

Barani Ulaya, katika nchi zinazotumia fedha ya Euro,uchumi umetabiriwa kushuka kwa asilimia 4.2.Katika nchi kama Uingereza hali hiyo itakuwa na maana ya kuongezeka kwa ukosefu waajiraa kwa asilimia 0.9 hadi kufikia mwishoni mwaka ujao.

Ujerumani imeshachukua hatua kadhaa ili kufufua uchumi wake.Lakini shirika laa fedha duniani IMF limetabiri uchumi wa nchi hii pia utashuka kwaasilimia 5.6 mnamo mwaka huu na asilimia moja zaidi mwaka ujao.

Jee Ujerumani inaweza kuchukua hatua zaidi.

Mtaalamu wa uchumi Jörg Decrassin ameeleza kuwa ''Ujerumani imeshachukua hatua za kufufua uchumi kwa kuingiza fedha katika mfumo. Kutokana na hayo bajeti yake ilikuwa na urari mnamo mwaka 2008 na kuingia katika nakisi ya asilimia 5 mwaka huu. Nakisi hiyo itaongezeka mwaka 2010 kwa asilimia sita ya pato jumla la ndani.''

Jee Ujerumani inaweza kuchukua hatua zaidi.?

Jibu ni ndiyo. Kwa sababu Ujerumani ina uwezekano wa kuchukua hatua zaidi.Haya ni mazingira ambapo serikali iliweka mipango mizuri wakati wa neema katika kurekebisha bajeti.''Hayo yanageuka kuwa manufaa katika nyakati ngumu". ameongeza Mtaalamu wa uchumi Jörg Decrassin

Shirika la IMF limeseam matumaini siyomakubwa sana mwaka ujao na limetabiri kutokuwepo an ustawi.Lakini limezitaka nchi zichuke hatua za haraka ili kuyasaidiamabenki na kutenga fedha zaidi ili kufufua uchumi na hivyo kufupisha kipindi cha kudorora kwa uchumi.


Mwandishi: Zawadzky,Karl/ZPR/A.Mtullya.

Mhariri: Josephat Charo