1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa Afrika Kusini washuka

Daniel Gakuba
7 Juni 2017

Uchumi wa Afrika Kusini umeshuka katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 na kusababisha ustawi wa taifa hilo lenye nguvu barani Afrika kudorora kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.

https://p.dw.com/p/2eF8F
Nov 27 2014 Cape Town South Africa View of the Gautrain inside Pretoria station Gautrain is
Picha: imago/ZUMA Press

Ukosefu wa ajira pia ukiwa umeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea kwa miaka 14, Rais Jacob Zuma anajikuta katika shinikizo kubwa la ama kuleta mabadiliko au kuhatarisha kupoteza nafasi yake. 

Wachambuzi wanasema takwimu zinaonyesha kwamba kunywea kwa uchumi katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kumetokana na udhaifu katika uzalishaji wa viwanda pamoja na biashara.

Vile vile ukosefu wa ajira na kutoongezeka kwa viwango vya mishahara kunaidhoofisha sekta ya wanunuzi ya Afrika Kusini iliyokuwa imara kwa muda mrefu.