1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchambuzi wa Magazeti ya Ujerumani

28 Mei 2008

Miongoni mwa mada zilizoshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo hii ni mgomo wa wafuga ngombe wa maziwa na msimamo wa kiongozi wa chama cha Social Demokratk SPD unaowayawaya.

https://p.dw.com/p/E7aC
Landwirt Thomas Bijamin verfüttert am Dienstag (27.05.2008) auf seinem Hof in Hahn-Lehmden bei Rastede Milch an seine Bullen. Mit einem Lieferboykott haben Deutschlands Bauern ihrer Wut über zu niedrige Milchpreise Luft gemacht. Von zahlreichen Höfen mussten die Wagen ohne Milch in die Molkereien zurückkehren. Man wolle erst wieder liefern, wenn man die Zusage für kostendeckende Preise erhalte, teilte der Bundesverband deutscher Milchviehhalter mit. Foto: Carmen Jaspersen dpa/lni +++(c) dpa - Bildfunk+++
Ngómbe wakipewa maziwa na Mkulima Thomas Bijamin aliegoma kuuza maziwa yake kwa bei ya chini ya hivi sasa.Picha: picture-alliance/ dpa

Tunaanza na mgomo wa wakulima.Gazeti la BILD ZEITUNG kutoka Berlin linasema:

"Mamilioni ya wanunuzi wanalalamika kuhusu bei za vyakula zinazozidi kuongezeka.Lakini wakulima wanaona ni bora wamwage maziwa yao kuliko kuuza kwa bei ya chini kabisa.Ukweli ni kwamba bei za maziwa na siagi hazikutulia,kwani katika kipindi cha miezi michache iliyopita bei hizo ziliongezeka kwa asilimia 50 na baadae zikateremka.

Kwa maoni ya DER NEUE TAG,mgomo wa wakulima hao ni ushujaa wa wale waliovunjika moyo.Kwani hakuna anaependa kumwaga chakula.Gazeti la NORDSEE-ZEITUNG kutoka Bremerhaven linasema:

"Wakulima hawawezi kuendelea kuuza maziwa yao kwa bei za hivi sasa.Inafaa kukumbuka kuwa mifugo inapowekwa katika hali zinazozingatia kuhifadhi mazingira na hali ya hewa wakulima hupata gharama zaidi kuliko wale wanaowafungia ndani ng´ombe wao.Kwa hivyo anaetaka cha rahisi basi awe tayari pia kula kile kinachotoka kule ambako mifugo huwekwa katika hali zinazopingwa na wanunuzi wengi.Ni bora kulipa bei inayostahilika badala ya kula kile kischokuvutia.

Kwa maoni ya WESTDEUTSCHE ZEITUNG wakulima wakikabiliana na gharama zinazozidi kuongezeka,hawakuona njia nyingine yo yote ya kulalamika isipokuwa kugoma.Lakini mgomo huo utakuwa na athari zake.Baadhi ya wakulima hao huenda wakalazimika kufunga kabisa biashara zao.Na hilo halitowasaidia wanunuzi hata kidogo.

Hebu sasa tugeukie mada nyingine.Kurt Beck alie kiongozi wa chama cha Social Demokratik-SPD katika siku za hivi karibuni ametokeza mara kwa mara katika magazeti ya Ujerumani.Kwa maoni ya STUTTGARTER NACHRICHTEN kuwayawaya kwake ni kama kitambulisho cha kiongozi huyo. Kwani kama majuma matatu yaliyopita kiongozi huyo wa SPD alipendekeza mpango mpya wa kodi,uliowapa wananchi matumaini ya kupunguziwa kodi.Lakini sasa,hilo si suala linalojadiliwa tena.Kinyume na hapo awali,kiongozi huyo sasa anazungumzia kuwatoza kodi zaidi hasa wale wenye pato la juu.

NORDWEST ZEITUNG linauliza:Chama cha SPD kinataka nini hivi sasa?Je,kinataka kuyakabili matatizo ya nchi, kama mshirika katika serikali ya muungano wa vyama vikuu?Au kina hamu ya kuwa upande wa upinzani na hivyo kujichimbia kaburi?Moja ni dhahiri,kwa hivi sasa hakuna jawabu lililo rahisi kwa chama cha SPD.Hayo ni maoni ya NORDWEST ZEITUNG.