1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchambuzi: Sharm-el-Sheikh

26 Juni 2007

Matokeo ya mkutano wa jana huko Sharm el-sheikh,misri kati ya waziri mkuu wa Israel na Kiongozi wa Palestina ni haba na kwamba hayakugusia maswali hasa yanayozitenganisha pande hizo mbili-adai Peter Philip:

https://p.dw.com/p/CHCE

Mkutano wa jana huko Sharm el Sheikh,nchini Misri kati ya waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Mamlaka ya ndani wa Palestina Mahmoud Abbas ulikuwa wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu miezi kadhaa.

Mkutano huo ambao pia walihudhuria rais Hosni Mubarak wa Misri na Mfalme Abdullah II wa Jordan,ulifanyika chini ya kivuli cha kunyakuwa madaraka kwa chama cha hamas katika mwambao wa Gaza.Matokeo ya kikao hicho cha Sharm el Sheikh si ya kuvutia .

Matokeo ya kikao cha jana ni tangazo la waziri mkuu wa Israel kuwaacha huru wafungwa 250 wafuasi wa chama cha FATAH.Kwa tangazo hilo waziri mkuu Olmert hakutia chumvi alipoonya tangu kabla pasitarajiwe makubwa kutoka Sham el Sheikh.

Kuwaacha huru wafungwa hao wa kipalestina hakukuwa matokeo ya majadiliano ,bali ni ishara ya nia njema upande wa Israel.Kwa kweli, Israel ilistahiki kumridhia mengi zaidi kiongozi huyo wa Palestina.

Kwani Israel imewaweka korokoroni kiasi cha wafungwa 10.000 wa kipalestina na kuwaacha huru 250 ni sawa na 2.5%.

Kikao hiki kati ya waziri mkuu Olmert na Mahmud Abbas hakijagusia maswali haya ya kimsingi .Azma hasa ilikua kumtia shime na kumpa nguvu Mahmud Abbas pamoja na kubainisha sio tu Israel,bali hata Jordan na Misri ziko nyuma ya Mahmud Abbas katika changamoto na chama cha Hamas.Hata lile kundi la pande 4 juu ya mzozo wa Mashariki ya kati linalokutana leo hii mjini Jeruselem,lina azma ya kutoa risala kama hiyo.

Iliobaki sasa ni kujua iwapo risala hiyo na nia njema zinatosha kuifikia shabaha inayotakiwa ?

Baada ya kinyan’ganyiro cha madaraka na Hamas katika mwambao wa Gaza kuamuliwa wazi kwa ushindi wa Hamas,Mahmud Abbas ameamua kufuata mkondo wazi wa kupinga matumizi ya nguvu n a kuendeleza utaratibu wa kusaka amani na Israel.

Amevuna ridhaa tangu ya Israel hata ya kambi ya magharibi.Iliobakia sasa kupata ridhaa pia ya wapalestina kuwa wako nyuma yake.Wengi wao lakini zamani wamekata tama kuwa njia ya amani yawezekana kabisa au iwapo italeta manufaa yoyote kwao.Ili kuwafufulia matumaini hayo,Mahmud Abbas anabidi kuamua lakini pia atahitaji kusaidiwa.

Hakuna kiovu zaidi kuliko kubainika ni kibaraka wa Israel au wa kambi ya magharibi.Mahmud Abbas anahitaji kutambuliwa kuwa mshirika barabara katika meza ya mazungumzo na muhimu kabisa anabidi kuonesha matokeo.

Kuwaacha huru wafungwa 250 kutapokewa mikono miwili na jamaa zao majumbani,lakini si mafanikio yanayotarajiwa isipokua ni kama sadaka tu iliotoa Israel.Israel itapaswa kufanya zaidi.

Ingelikuwa bora siku zijazo kuacha huru wafungwa kuwe zao la mazjngumzo na sio huruma kutoka upande mmoja.Pia haitatosha ikiwa Israel sasa itaanza kuziachia fedha za kodi za wapalestina ilizozizuwia mwaka mmoja na nusu uliopita.Fedha hizo tangu hapo, si mali ya Israel na ilikua kitambo izikabidhi mikononi mwa wapalestina.Haikufanya hivyo ili kutoimarisha serikali ya HAMAS.

Muhimu sasa, ni kusaka mbinu ya ufumbuzi wa mzozo huu mzima na wapalestina.Ufumbuzi huo uchukue sura gani ajua kila mmoja kitambo sasa: paundwe dola la wapalestina kandoni mwa dola la Israel tena katika mipaka yake iliokuwapo kabla ya vita vya 1967.

Na Mahmud abbas ameitisha pafanyike mazungumzo ya maana kuelekea shabaha hiyo na kundi la pande 4 linakutana leo jeruselem,litapaswa kumuungamkono.Shauri la Saudia Arabia lafaa kuitikiwa –shauri ambalo linaiahidi Israel amani endapo itan’gatuka kutoka ardhi ilizozikalia.Israel, imenyamaa kimya hadi sasa,labda ingefaa kulisikiliza shauri hilo.