1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa wabunge Iraq

7 Machi 2010

Uchaguzi wa Iraq umeanza rasmi hii leo . Shughuli ya uchaguzi wa wabunge nchini Iraq imegubikwa na milipuko kadhaa na mashambulio ya makombora baada ya kundi la Al-Qaeda tawi la Iraq kutishia kuivuruga pamoja na kuwaua

https://p.dw.com/p/MMOT
Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki anayewania wadhifa huo tenaPicha: AP

Kiasi cha watu 26  wameuawa mjini Baghad,  hii leo baada ya mabomu kulipuka katika maeneo kadhaa.Mashambulio hayo yanavyovilenga  vituo vya kupigia kura yameripotiwa pia kutokea katika miji miengine.Zaidi  ya wagombea alfu 6 wanawania viti 325 katika Baraza la Wawakilishi wakiwemo wanawake 1.718.Waziri Mkuu aliye madarakani ambaye ni kiongozi wa chama cha madhehebu ya Shia cha State of the Law Alliance, anawania tena wadhifa huo.Kiasi cha askari polisi na wanajeshi wanapiga doria ili kuwahakikishia wapiga kura usalama.Hii ni mara  ya pili, Iraq inafanya uchaguzi tangu utawala wa Saddam Hussein, kuangushwa mwaka 2003 na una azma ya kuutathmini ustawi wake. 

Selbstmordanschlag in Baghdad, Irak
Hali mbaya baada ya mlipuko wa bomu BaghdadPicha: AP