1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa ushindani mkali kuwahi kushuhudiwa Gabon

27 Agosti 2016

Wananchi wa Gabon Jumamosi (27.08.2016) wamejitokeza katika uchaguzi atakaokuwa na ushindani mkali kabisa kuwahi kumkabili Rais Ali Bongo ambaye familia yake imeidhibiti nchi hiyo kwa takriban nusu karne.

https://p.dw.com/p/1JqyD
Picha: Getty Images/AFP/M. Longari

Bongo mwenye umri wa miaka 57 alishika madaraka hapo mwaka 2009 wakati baba yake Omar alipofariki dunia hapo mwaka 2009 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 42 na alisdhinda katika uchaguzi mwaka huo huo.Vyombo vya dola na mitandao iiliyojikita yenye kumpendelea vyote hivyo vikililainishwa na utajiri wa mafuta wa nchi hiyo Bongo yumkini akashinda tena safari hii.

Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa kumi na mbili jioni lakini matokeo hayatarajiwi kutolewa hadi Jumatatu au Jumanne.Mipaka ya bahari na ya ardhini imefungwa Ijumaa usiku na itaendelea kufungwa hadi Jumamosi usiku.

Bongo anakabiliana na wagombea wengine tisa kulinganisha na 22 aliyokabiliana nao katika uchaguzi wa mwisho lakini kivumbi kiko kwa mshindani wake mkuu Jean Ping mwenye umri wa miaka 73 ambaye anaitumia hali ya kutoridhika kwa umma na hali ya mbaya ya maisha licha ya utajiri mkubwa wa mafuta ilionayo nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni wasiozidi milioni mbili.

"Wananchi wa Gabon wanateseka.Hatulipwi vizuri watoto ,wetu hawaishi katika mazingira mazuri. Ndio maana nimepiga kura ya mabadiliko." Ametamka hayo Marie Ange N'no mwenye umri wa miaka 40 mtumishi wa serikali akiwa nje ya kituo cha kupiga kura katika mji mkuu wa Libreville lakini amekataa kusema amempigia kura nani.

Nchi tajiri wananchi maskini

Gabon ambayo hivi karibuni tu imejiunga tena na Shirika la Nchi Zenye kuzalisha mafuta kwa wingi duniani (OPEC) baada ya kutokuwepo kwa miongo miwili,pato lake la jumla la taifa kwa kila mtu kwa mwaka ni dola 10,000 na kuifanya nchi hiyo kuwa mojawapo ya nchi tajiri kabisa barani Afrika lakini bado takriban theluthi ya wananchi wake wanaishi chini ya mstari wa kiwango cha ufukara cha taifa.

Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon.
Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon.Picha: picture-alliance/dpa/M. Yalcin

"Nataka kuanzisha mapambano bila ya huruma dhidi ya umaskini." Bongo amesema hayo hapo Alhamisi kwenye viunga vya Libreville."Lazima utoweke nchini mwetu na sitosita hadi hapo tumefanikisha hilo."

Lakini nchi hiyo inakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha kutokana na kushuka kwa muda mrefu uzalishaji wa mafuta pamoja na kuporomoka sana kwa bei ya mafuta ghafi katika kipindi cha miaka miwili iliopita.Juhudi za kuutanuwa uchumi wa nchi hiyo katika sekta za kilimo na utalii bado kuzaa matunda.

Utajiri wa mafuta unawanufaisha vigogo tu wa nchi hiyo kuna wakati Gabon ilikuwa ndio yenye kuagizia mvinjo wa shampeni kwa wingi duniani kwa kuzingatia kwa kila kichwa.

Wakati wa utawala wa baba yake,Gabon ilikuwa nguzo ya "La Francafrique" kundi la siri la mizengwe,la kidiplomasia na biashara na lenye uwezo wa kijeshi wa Ufransa ambalo huwadumisha maimla wa Kiafrika madarakani na kuzipatia kazi kampuni za Kifaransa.

Bongo amekuwa akijaribu kuondokana na haiba hiyo aliyoiacha baba yake kwa kuwasilisha taswira mpya ya miradi ya maendeleo inayosimamiwa na wasomi.

Lakini upinzani umekuwa ukielekeza zaidi shutuma zake kwa Ali Bongo kwa madai kwamba yeye ni mtoto wa kusaili kutoka eneo la mashariki mwa Nigeria na kwamba hastahiki kuongoza nchi madai ambayo anayakanusha.Hata hivyo hali ya mvutano kati ya pande hizo mbili inaweza kutokota na kuwa vurugu.

Tuhuma za upinzani

Ping ambaye ni mwana wa kiume aliechanganya damu wa mfanya biashara tajiri wa Kichina ni waziri wa mambo ya nje wa zamani na mwenyekiti wa zamani wa halmashauri ya Umoja wa Afrika aliwahi kuwa mtu wa karibu kwa Omar Bongo na pia kuwa na uhusiano na binti yake Pascaline ambaye amezaa naye watoto wawili.

Mpinzani mkuu Jean Ping.
Mpinzani mkuu Jean Ping.Picha: Reuters

Lakini alihitilafiana na "Bongo Junior" kama wananchi wa Gabon wanavyomwita rais wao na amejitowa katika chama tawala hapo mwaka 2014 na kuja kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali.

Ping anakabiliwa na kibaruwa kigumu mojawapo ya sababu ni kwamba mfumo wa duru moja ya uchaguzi nchini Gabon inamaanisha mshindi hahitaji ushindi wa wingi wa kura ili mradi kura zake zinampita mwenzake.Mara ya mwisho Bongo alishinda kwa asilimia 41.73 tu ya kura.

Mhariri : Mohamed Dahman/Reuters/dpa

Mhariri : Caro Robi