1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya waanza

Admin.WagnerD22 Mei 2014

Mataifa ya Uholanzi na Uingereza leo hii yanafungua uwanja wa mapambano katika uchaguzi wa bunge jipya la Umoja wa Ulaya. Mataifa mengine yatafuata mkondo huo na matokeo yatatolewa jumapili.

https://p.dw.com/p/1C4Si
Europawahl Niederlande 22.05.2014
Wapiga kula wakishiriki wajibu huo nchini UholanziPicha: Reuters

Bunge la Umoja wa Ulaya linashikilia rekodi ya kuwa na idadi kubwa ya wabunge. Bunge hilo kubwa duniani linalochaguliwa kupitia mchakato unaofanyika kwa njia ya uhuru na haki linatarajiwa kuwa na wabunge 751. Bunge hili linatajwa pia kuwa ni la kipekee na kidemokrasia lenye kuwawakilisha raia milioni 504 wa Umoja wa Ulaya.

India ambayo ilifanya uchaguzi wake wa bunge hivi karibuni ina idadi ya watu mara mbili ya hao lakini bunge lake bado dogo likiwa na wawakilishi 543 wa viti vya ubunge. Bunge la Ulaya kwa wakati huu linauwezo mkubwa kama wa baraza, lenye kujumuisha watendaji kutoka mataifa 28 wanachama.

Kuzorota kwa uchaguzi

Pamoja na kuwa na nguvu kubwa mabadiliko katika mchakato huo wa uchaguzi ni muhimu. Idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura imeendelea kupungua ambapo kwa uchaguzi wa mwisho wa 2009 kiasi ya wapiga kura asilimia 43 tu ndio waliojitokeza katika vituo vya kupiga kura.

Martin Schulz mgombea wa juu kabisa katika kinyang'anyiro hicho kutoka upande wa chama cha kisoshalisti aliiambia DW kwa kifupi uchaguzi kwa hivi sasa umepooza. Amesema kwa hivi sasa wanataka kufanya kwa namna tofauti. Vyama vyote vikubwa vimetoa mgombea kuwania nafasi ya urais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya. hiyo ni nafasi yenye ushawishi mkubwa katika utawala wa umoja huo katika ofisi zilizopo mjini Brussels, Ubelgiji. Ofisi hiyo inawajibika katika udhibiti wa mikataba ya Umoja wa Ulaya na vilevile inaweza kupendekeza kanuni.

Europawahl Grobritannien Nigel Farage 22.05.2014
Kituo cha kupigia kura nchini UingerezaPicha: Reuters

Kampeni za uchaguzi

Ikiwa zinaaminiwa tathimini za kisayansi kampeni ya urais wa kamisheni ya umoja huo bado haijaanza ingawa vyombo vya habari vya Ujerumani, Ufaransa,Ubelgiji na Italia vimeonesha sana harakati za wagombea wakuu wa kinyang'anyiro hicho.

Martin Schulz na mpinzani wake mhafidhina Jean-Claude Juncker, ambae alikuwa waziri mkuu wa Luxembourg wana wakati mgumu ya kuvutia wapiga kura. Katika wakati huu kukiwa na kiwango kikubwa cha tatizo la ajira na sera kali za kubana matumizi katika mataifa mengi, watafiti katika masuala ya uchaguzi wanatarajia kutokea ushindani mkubwa.

Jean-Claude Juncker na Martin Schulz Spitzenkandidaten Europawahl TV-Debatte 20.05.2014
Wagombea nafasi ya urais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker na Martin SchulzPicha: Reuters

Wetu wenye kuegemea mrengo wa shoto au kulia watashinda huko Ufaransa, Uingereza, Uholanzi,Finland, Italia na Ugiriki. Kwa makadirio moja ya tano ya viti vya ubunge vitakwenda kwa wanasiasa wenye msimamo mkali.

Baada ya uchaguzi huu wa bunge, kitakachofuata kukubaliana kwa pamoja kuhusu rais wa kamisheni ambapo wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya watakutana katika baraza la Umoja wa Ulaya.

Mwandishi:Bernd Riegert/tafsiri Sudi

Mhariri:Yusuf Saumu