1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Hessen

Oumilkher Hamidou19 Januari 2009

Wapiga kura wa Hessen hawataki hadaa

https://p.dw.com/p/GbJC
Waziri mkuu wa zamani,wa muda na mpya Roland KochPicha: AP



 Mada mojawapo magazetini hii leo ni kuhusu ugomvi wa Mashariki ya kati.Lakini bila ya shaka mada iliyohanikiza zaidi ni kuhusu uchaguzi wa bunge katika jimbo la Hessen.Na gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaamini kwamba:


TSG,au Thorsten Schäfer-Gümbel,hana lawama,tenas hata kidogo.Mgombea huyo wa chama cha SPD sio sababu.Mwanasiasa huyo ambae miezi mitatu iliyopita,hakuna aliyekua akimjua na ambae  miezi miwili na nusu  tuu hivi amepanda katika jukwaa la kisiasa kama mwanafunzi wa Yipsilanti,amejitahidi awezavyo.Lakini jahazi ilikua inakwenda mrama na Thorsten Schäfer-Gümbel asingeweza kuizuwia isizame.Jana SPD wamejipatia onyo kwa kuvunja ahadi ,kwa kiburi na ujinga,na onyo kwa mbinu za kutaka kwa kila hali kutwaa madaraka.Ushindi uliopatikana uchaguzi ulipoitishwa January mwaka jana umegeuka pigo lisilokua na mfano,mwaka mmoja baadae.Aliyeshindwa hasa ni Andrea Yipsilanti.Amepuuza matakwa ya wapiga kura na kupitisha maamuzi bila ya kushauriana na viongozi wenzake chamani."


Gazeti la RHEIN-NECKER-ZEITUNG la mjini HEILDELBERG linahisi:


"Ni nadra kuona wanasiasa wenye kiburi na wasiotaka kujifunza wakiadhibiwa kama ilivyoshuhudiwa huko Hessen.Mbio za Yipsilanti zimemalizikia sakafuni.Zimemalizika kwa onyo la wapiga kura:Sio kila mbinu zinahalalisha lengo la kisiasa.Kilichoibuka na ushindi ni usemi wa chama cha FDP,"tulichoahidi tutakitekeleza"


Wana SPD wanajikosoa huku jimbo la Hessen likiendelea kutawaliwa na waziri mkuu ambae walio wengi hawamtaki-linatathmini gazeti la SCHWERINER VOLKSZEITUNG hali jumla namna ilivyo huko Hessen na kuendelea kuandika:


"Roland Koch,kufumba na kufumbua kaachana na  malumbano ya chuki dhidi ya wageni,anastahiki kuwashukuru wana SPD na vichwa mchungu ,kwasababu sasa anaweza kuunda serikali ya muungano pamoja na waliberali wa FDP.Kimsingi, CDU wamejikingia kura chache tuu za ziada-na ukitilia maanani idadi ndogo ya walioteremka vituoni,basi hutokosea ukisema CDU wamepoteza wapiga kura.Kwamba CDU hawakuweza kufaidika na zilzala iliyokitikisa chama cha SPD,hali hiyo haiwezi na wala haitomridhisha Ronald Koch.Muhimu lakini kwa sasa  ni kuona hatimae jimbo la Hessen linaajipatia serikali imara."



Mada ya pili magazetini inahusu hali ya Mashariki ya kati ambako Israel na Hamas wametangaza kuweka chini silaha.Gazeti la Die Welt linaandika:


"Viongozi wa Umoja wa Mataifa na nchi za magharibi wamepania. Wanazungumza lakini wanafikiria  ufumbuzi wa muda tuu.Huo hausaidii kitu.Mada muhimu zaidi inayobidi kushughulikiwa ni uungaji mkono wa makundi ya kidini,na hapa ni kundi la itikadi kali ya dini ya kiislam.Si jambo linaloweza kuvumiliwa kuona wakuu wa Hamas wanaishi Damascus na kutoka huko wanatoa matamshi ya chuki dhidi ya Israel na ulimwengu wa magharibi.Muhimu zaidi ni matamshi ya chuki yanayosikika kutoka misikitini na kupitia vituo vya matangazo ya kiarabu tangu vya televisheni,Radio mpaka mtandao wa Internet. Ndio maana viongozi wa kisiasa na kanisa wa nchi za magharibi wanawajibika kutumia ushawishi wao.Pale tuu maimam watakapoacha kutukuza mauwaji,ndipo amani ya kweli itakapopatikana katikia ardhi tukufu.