Uchaguzi mkuu wafanyika leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.11.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uchaguzi mkuu wafanyika leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Uchaguzi wa leo unafuatia kampeni iliyogubikwa na machafuko ambapo watu wawili waliuwawa siku ya mwisho ya kampeni. Mji wa Lubumbashi ulikuwa kitovu cha machafuko kuelekea uchaguzi.

default

Wafuasi wa upinzani wakiandamana kabla uchaguzi wa leo

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inafanya uchaguzi mkuu hii leo. Uchaguzi huo unafanyika licha ya kuwepo hofu kuwa ungecheleweshwa kutokana na matatizo ya utaratibu na usafirishaji wa vifaa vya kupigia kura. Miito ilitolewa na wakosoaji kutaka uchaguzi huo uchunguzwe upya kutokana na kasoro zilizojitokeza. Rais wa sasa, Joseph Kabila, anashindana na wagombea wengine 10 kuwania wadhifa wa urais, huku wagombea 18,500 wakishindania viti 500 vya ubunge. Mkuu wa tume huru ya uchaguzi nchini humo, Daniel Ngoy Mulunda, alisema jana kwamba nchi hiyo itaandaa uchaguzi wa amani na halali na kudhihirisha kwamba wakosoaji wa mchakato mzima wa uchaguzi huo walikosea katika kutoa tathmini yao.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

Mhariri: Mohammed Khelef

 • Tarehe 28.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13IFr
 • Tarehe 28.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13IFr

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com