1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi katika mikoa ya Ujerumani-Hesse na Niedersachsen

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyJJ

WIESBADEN: Nchini Ujerumani leo kunafanywa uchaguzi wa bunge katika mikoa miwili ya Magharibi-Hesse na Niedersachsen.Uchaguzi wa mabunge ya mikoa hiyo miwili ni mtihani kwa Kansela Angela Merkel na chama chake cha CDU,kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.Chama cha CDU kinatawala peke yake mkoani Hesse tangu kushinda uchaguzi wa mkoani mwaka 2003 kwa kujinyakulia asilimia 49 ya kura. Leo,mgombea wa chama cha SPD Andrea Ypsilanti anatazamia kukiimarisha chama chake kilichopata pigo kubwa katika uchaguzi wa mwaka 2003 baada ya kujinyakulia asilimia 29 tu ya kura.

Matokeo ya uchaguzi wa leo katika mkoa wa Hesse yanangojewa kwa hamu kubwa,baada ya matamshi ya waziri mkuu wa mkoa huo Roland Koch kuhusu uhalifu wa vijana wa kigeni kuzusha mabishano makali wakati wa kampeni za uchaguzi.

Lakini katika mkoa wa Niedersachsen,uchunguzi wa maoni umeonyesha kuwa Waziri Mkuu wa mkoa huo,Christain Wulff wa chama cha CDU ana nafasi nzuri ya kubakia madarakani katika serikali ya mseto pamoja na chama cha FDP.Wakati huo huo katika mikoa yote miwili kunangojewa kwa hamu vipi chama cha Die Linke kitajitokeza hii leo.Chama hicho hakijawahi kuwakilishwa bungeni katika mikoa ya magharibi.