1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Japan wafungua ukurasa mpya

31 Agosti 2009

Wapiga kura Japan wamekiadhibu vikali chama tawala cha "Liberal Democratic Party" LDP katika uchaguzi uliofanywa siku ya Jumapili. Chama hicho kimepoteza viti 181 kwa hivyo sasa kinaingia bungeni kikiwa na viti 119 tu .

https://p.dw.com/p/JM40
Prime Minister Taro Aso, leader of the Liberal Democratic Party, adjusts a earpiece during a TV interview while observing the result of the parliamentary elections ballot counting at the party headquarters in Tokyo Sunday, Aug. 30, 2009. Aso conceded defeat in elections Sunday as media exit polls indicated the opposition had won by a landslide, sending the conservatives out of power after 54 years of nearly unbroken rule amid widespread economic anxiety and desire for change. (AP Photo/Shuji Kajiyama)
Waziri Mkuu wa Japan, Taro Aso wa chama cha cha LDP.Picha: AP

Kwa upande mwingine chama cha "Democratic Party of Japan" DPJ kitakuwa na wajumbe 308 katika bunge lenye viti 480.

Uchaguzi wa jana nchini Japan umefungua ukurasa mpya katika historia ya nchi hiyo baada ya chama LDP kushindwa vibaya na kungolewa madarakani kufutia utawala wa zaidi ya miaka hamsini. Kiongozi wa chama hicho Waziri Mkuu Taro Aso akikubali kushindwa kwa chama chake alisema:

"Ninabeba dhamana kwa kushindwa kwa chama cha LDP. Chama changu na miye hatuna budi kukubali na kuutia maanani uamuzi wa umma. Tunapaswa kuanza upya. Na kama mwanachama wa kawaida wa LDP nitafanaya kila niwezalo kutekeleza kazi hiyo."

Waziri Mkuu Taro Aso amesema atajiuzulu kama kiongozi wa chama cha LDP baada ya chama hicho kushindwa vibaya kabisa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu kuundwa kwake zaidi ya miaka hamsini iliyopita. Amesema kuwa serikali yake imeshindwa kupata suluhu kwa matatizo yaliyokuwa yakikabiliwa na umma kwa miaka mingi. Hata mawaziri wake wamekiri kuwa sasa wameadhibiwa na wapiga kura.

Chama hicho kimelaumiwa na wananchi kuhusu mwanya wa pato uliozidi kuwa mkubwa,mfumo wa malipo ya uzeeni uliosambaratika na kashfa mbali mbali zilizokiandama chama cha LDP. Vile vile chama hicho kimelaumiwa kwa hali mbaya ya uchumi inayoshuhudia kwa mara ya kwanza nchini humo tangu Vita Vikuu vya Pili.

Kwa upande mwingine, kiongozi wa chama DPJ Yukio Hatoyama akiwashukuru wapiga kura amesema imechukua muda mrefu lakini sasa wameshawasili. Huu ni mwanzo kwani kuna kazi zinazongojea kufanywa.Amesema:

"Kwa mara ya kwanza katika historia ya katiba yetu wananchi wameleta mabadiliko barabara na wamechagua serikali mpya kwa ujasiri.Kama mjumbe wa chama cha DPJ natoa shukrani zangu. Sasa tutaanza kufanya kazi yetu kwa kuzingatia maslahi ya umma na kuheshimu wananchi."

Yukio Hatoyama, leader of the main opposition Democratic Party of Japan, adds a red rosette on the name of a winner candidate as he observes the ballot counting of parliamentary elections at the party's election center in Tokyo, Japan, Sunday, Aug. 30, 2009. The left-of-center Democratic Party was set to win 300 or more of the 480 seats in the lower house of parliament, ousting the Liberal Democrats, who have governed Japan for all but 11 months since 1955, according to exit polls by all major Japanese TV networks. (AP Photo/Koji Sasahara)
Mshindi wa uchaguzi wa Japan Yukio Hatoyama wa chama cha DPJ.Picha: AP

Chama cha DPJ kimeahidi kufufua uchumi wa Japani kwa mfano kwa kupunguza matumizi ya serikali yasio ya lazima na kuongeza pato la wafanyakazi ili kuhimiza matumizi. Uchumi utapewa kipaumbele na Yukio Hatoyama anaetazamiwa kuchaguliwa waziri mkuu mpya wa Japan katika mkutano maalum utakaofanywa katikati ya mwezi ujao wa Septemba.

Mwandishi:P.Kujath/ZPR/ P.Martin/RTRE

Mhariri:M.Abdul-Rahman