1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubelgiji yairarua Estonia 8-1

Sekione Kitojo
14 Novemba 2016

Ubelgiji yapitisha  mipira  mara  nane  katika  nyavu za Estonia , wakati  Cristiano  Ronaldo  apiga  mabao  mawili wakati  Ureno  yanusurika  kitisho  cha  Latvia kwa  kuizaba mabao 4-1.

https://p.dw.com/p/2SgJ3
Fußball WM-Qualifikation Portugal gegen Lettland
Cristiano Ronaldo wa UrenoPicha: Picture-Alliance/dpa/M. Cruz

Ubelgiji  iliikandika  Estonia  mabao 8-1 na  kujiweka  juu kabisa  ya  kundi  H  katika  kinyang'anyiro  cha  kuwania kukata  tikiti  ya  kucheza  katika  fainali  za  kombe  la dunia  mwaka  2018  nchini  Urusi, wakati  Cristiano Ronaldo  alipachika  mabao  mawili  wakati  Ureno ikichomoka  katika  kitisho  cha  Latvia   kabla  ya  kuirarua timu  hiyo  kwa  mabao  4-1  katika  mchezo  wa  kufuzu kukata  tikiti  ya  kucheza  katika  fainali  za  kombe  la dunia  jana  Jumapili.

Kwa  upande  wa  Ubelgiji Romelo Lukaku  na Dries Mertens  walifunga  mabao  ikiwa  ni  pamoja  na  Thomas Meunier , Eden Hazard , Yannick carrasco  pamoja  na  goli la kujifunga  wenyewe  na  kupata  ushindi  mara  nne katika  michezo  minne.

Katika  kundi  hilo  hilo  Ugiriki  ilipata  bao  la  kusawazisha katika  dakika  ya  95  kupitia  kwa  Giorgos Tzavellas baada  goli  la  kuongoza  la  Bosnia.

Pointi  moja  ya  Ugiriki  ina  maana  kwamba  Wagiriki sasa  wana pointi  10  kutokana  na  michezo  minne  katika kundi  H, mbili  nyuma  ya  Wabelgiji.

Ronaldo  alifunga  mabao  mawili  akakosa  penalti  wakati mabingwa  wa  Ulaya  Ureno  wakibakia  pointi  tatu  nyuma ya  viongozi  wa  kundi  B , Uswisi. Mapema  katika  kundi hilo  B Visiwa  vya  Faroe  walishindwa  kuhimili  vishindo vya  Uswisi  kwa  kukandikwa  mabao 2-0.

Katika  kundi  hilo  pia  Hungary  iliishindilia  Andora  kwa mabao 4-0.

Uholanzi  iliishinda  Lexemburg  kwa  mabao  3-1  katika kundi  A, wakati  pia  katika  kundi  hilo Bulgaria  ilikaba koo Belarus  kwa  kuifunga  bao 1-0.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo
Mhariri: Yusuf  Samu