1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubalozi wa Ujerumani mjini Khartoum washambuliwa

14 Septemba 2012

Maelfu kwa maelfu ya waislamu wameandamana katika kila pembe ya ulimwengu wa kiarabu na Asia baada ya sala ya Ijumaa. Machafuko yameripuka miongoni mwa kwengineko nchini Sudan ambako Ubalozi wa Ujerumani umetiwa moto.

https://p.dw.com/p/169F8
A Sudanese demonstrator burns a German flag as others shout slogans after torching the German embassy in Khartoum during a protest against a low-budget film mocking Islam on September 14, 2012. Around 5,000 protesters in the Sudanese capital angry over the amateur anti-Islam film stormed the embassies of Britain and Germany, which was torched and badly damaged. AFP PHOTO / ASHRAF SHAZLY (Photo credit should read ASHRAF SHAZLY/AFP/GettyImages)
Sudan Khartum Angriff auf deutsche BotschaftPicha: AFP/Getty Images

Mjini Khartoum wafuasi wasiopungua elfu tano wa itikadi kali ya dini ya kiislamu wamezivamia ofisi za balozi za Uingereza na Ujerumani na kuutia moto ubalozi wa Ujerumani. Kwa mujibu wa mashahidi na maripota wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, na lile la Ufaransa, AFP, waandamanaji waliojaa hasira waliparamia jengo la ubalozi wa Ujerumani na kupandisha bendera ya itikadi kali badala ya ile ya Ujerumani.

"Watumishi wa ubalozi wako salama" amesema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, aliyewataka maafisa wa serikali ya mjini Khartoum wachukue hatua zinazohitajika kudhamini usalama wa wanadiplomasia.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/Reuters

Mhariri:Josephat Charo