Tzipi Levny huenda akaongoza ujumbe wa Israel katika mazungumzo yajayo ya amani | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tzipi Levny huenda akaongoza ujumbe wa Israel katika mazungumzo yajayo ya amani

Jerusalem

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameamua kumteuwa waziri wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni kuongoza ujumbe wa Israel katika mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati mwezi ujao nchini Marekani.Kulingana na vyombo vya habari vya Israel,waziri mkuu Olmert huenda akatangaza uamuzi huo hii leo,wakati wa mkutano wa kila wiki wa baraza lake la mawaziri.Hadi wakati huu wahariri wa kisiasa nchini Israel walikua wakiamini ,kiongozi wa pili serikalini Haim Ramon angechaguliwa kuongoza ujumbe wa Israel mazungumzoni.Kuteuliwa bibi Tzipi Livni kunaashiria msimamo mkali unaoweza kufuatwa na Israel katika mazungumzo hayo .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com