1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuzo ya amani ya mashirika ya kuchapisha vitabu ya Ujerumani atunukiwa muandishi kitabu mwenye asili ya Israel

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fo

Frankfurt Am Main:

Mtu anaesemekana akili yake si nzuri, alijaribu kutaka kumshambulia rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Horst Köhler mjini Frankfurt.Bwana mmoja mwenye umri wa miaka 44 alimvuta ukosi wa koti rais Köhler kabla ya kudhibitiwa na walinzi .Msemaji wa polisi amesema rais Horst Köhler hakujeruhiwa na aliendelea kushiriki katika hafla ya tuzo ya amani ya mashirika ya wachapisha vitabu wa Ujerumani katika kanisa la Paul mjini Frankfurt.Tuzo ya mwaka huu ametunukiwa mtaalam wa Taareh wa kutoka Israel,Saul Friedländer.Mtaalam huyo wa historia mwenye umri wa miaka 75 amekabidhiwa tuzo hiyo yenye thamani ya yuro 25 elfu kutokana na ufafanuzi wa kitabu chake „Enzi ya tatu na wayahudi“ akichambua mauwaji ya halaiki ya wayahudi yaliyofanywa na wanazi katika vita vikuu vya pili vya dunia –Holocaust,kati ya mwaka 1933 na 1945.