Tunisia yafanya uchaguzi wa kwanza huru | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.10.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tunisia yafanya uchaguzi wa kwanza huru

Watunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza kufuatia "Uasi wa Majira ya Machipuko katika Nchi za Kiarabu"miezi tisa baada ya maandamano ya vuguvugu la umma kumn'gowa madarakani Rais Zine al- Abidine Ben Ali.

default

Waandamanaji wakiwa na bendera ya Tunisia wakati wa vuguvugu la umma lililompinduwa Rais Zine Ben Ali wa nchi hiyo.

Uchaguzi huo ambao ni wa kwanza huru katika historia ya Tunisia utaweka mfano kwa nchi nyengine za Kiarabu ambapo uasi umechochea mabadiliko ya kisiasa.Tunisia ndio ilioanzisha "Vuguvugu la Majira ya Machipuko ya Nchi za Kiarabu" miezi 10 iliopita wakati maandamano ya umma kupinga umaskini,ukosefu wa ajira na ukandamizaji wa serikali yalipomlazimisha Rais Ben Ali kukimbilia Saudi Arabia. Uchaguzi wa leo ni wa baraza la katiba ambalo litarasimu katiba mpya na pia kuteua serikali ya mpito na kupanga uchaguzi wa rais na bunge nchini humo.

 • Tarehe 23.10.2011
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RsT0
 • Tarehe 23.10.2011
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RsT0

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com