1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya muda ya uchaguzi Kenya imejiandaa kwa kura ya maoni Agosti 4

Josephat Nyiro Charo2 Agosti 2010

Kampeni zote hazitaruhusiwa kuanzia leo usiku, iwe ni kupitia mikutano ya hadhara au matangazo kwenye redio na televisheni

https://p.dw.com/p/OaJt
Ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 Kenya. Je kura ya maoni itakuwaje?Picha: AP

Tume ya uchaguzi nchini Kenya imo katika maandalizi ya mwisho kabla tayari kwa kura ya maoni itakayopigwa Jumatano ijayo, kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo. Tume hiyo imesema kwamba kuanzia leo usiku hakutaruhusiwa mipango yoyote ya kampeni hadharani wala faraghani.

Kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kitaifa, tume hiyo itatumia mbinu ya simu ya mkononi kupokea matokeo kutoka katikavituo vyote vya kupigia kura ili kuharakisha zoezi hilo. Peter Moss alizungumza na kamishna wa tume hiyo ya uchaguzi Winnie Guchu na alianza kwa kueleza mikakati yao ya kujitayarisha.

Mwandishi, Peter Moss

Mhariri, Abdul-Rahman Mohamed