Tukio 19 – Kuingilia Jambo kwa Kina | Radio D Teil 1 | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 19 – Kuingilia Jambo kwa Kina

Ingawa maduara ya mimea yalitengezwa na Wakulima, Eulalia bado anaamini kuna madude yanayoanguka kutoka angani. Katika kuchunguza ulaghai huo, Philipp na Paula wanakwenda baa ya mahali ambako wanazungumza na wanakijiji.

Waandishi habari waenda kwenye baa.

Waandishi habari waenda kwenye baa.

Paula na Philipp wametengua kitendawili cha maduara ya mimea lakini bado wana shaka kuhusu kuweko kwa madude yanayoanguka kutoka angani. Madude hayo ni nini? Eulalia anasisitiza amewahi kuliona moja. Hatimaye waandishi habari hao wanawauliza wateja kwenye baa maoni yao kuhusu maduara bandia ya mimea.

Ziara ya baa ni fursa nzuri ya kutanguliza wakati uliopita, hasa kitenzi kisichotabirika "sein" (kuwa). Kitenzi cha utaratibu "können" (kuweza) pia kimeangaziwa katika tukio hili. Zingatia jinsi irabu zinavyobadilika wakati wa kunyambua kitenzi.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa