Tukio 06 – Mfalme Ludwig alifariki vipi? | Radio D Teil 1 | DW | 24.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 1

Tukio 06 – Mfalme Ludwig alifariki vipi?

Katika Kasri la Neuschwanstein, Paula na Philipp wanakutana na mgeni wasiyemwelewa ambaye amevaa joho la Mfalme Ludwig. Wanafanya uchunguzi kuhusu utata unaogubika kifo cha Ludwig.

Nani anavaa joho la Mfalme Ludwig?

Nani anavaa joho la Mfalme Ludwig?

Mwanamume aliyejitanda mabegani mwake joho la Mfalme Ludwig anajaribu kuwasadikisha Paula na Philipp kwamba yeye ni marehemu mfalme. Je Ludwig alifariki vipi? Waandishi hao wawili wa habari wanatayarisha mchezo wa redio kuwaeleza wasikiliza wao kuhusu nadharia kadha wa kadha za kifo cha Mfalme Ludwig katika Ziwa la Starnberg. Hakuna anayejua kwa uhakika ikiwa aliuliwa au alijiua.

Mkutano na mtu huyo asiyeeleweka ni fursa nzuri ya kusikia tofauti za kawaida zilizopo kati ya kuzungumza na rafiki au mgeni. Sikiliza kiwakilisha rasmi "Sie" na kiwakilishi kisicho rasmi "du." Kitenzi-jina cha kitenzi "kuwa" – "sein" ni.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa