1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TRIPOLI-Nchi za Ulaya na Afrika zakubaliana juu ya swala la wahamiaji haramu

Mawaziri kutoka nchi za Ulaya na Afrika waliokuwa wakikutana mjini Tripoli- Libya, wamekubaliana juu ya swala la wahamiaji haramu kwa kulishughulikia kwa hatua za kiusalama sambamba na hatua za kufikia malengo ya kimaendeleo. Katika taarifa ya pamoja, mawaziri wamesema swala la wahamiaji haramu haliwezi kusuluhishwa kwa hatua za usalama pekee. Wamesema malengo yatakuwa kupambana na umasikini, ukosefu wa uajira na kuenea magonjwa kwa dhamira la maendeleo ya kudumu.

Umoja wa Ulaya umependekeza kutumia mfumo wa vigezo vya wahamiaji watakaoruhisiwa kuingia katika nchi wanachama kulingana na mahitajio ya soko la ajira na vile vile kutekeleza ahadi ya kuongeza misaada ya maendeleo kwa nchi masikini hadi asili mia 0,56 ya pato la nchi kufikia mwaka 2010 na halafu hadi asili mia 0,7 kufikia mwaka 2015.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com